Abiria kadhaa akiwemo Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, wamenusrika kifo baada ya ndege walimokuwa ya Precision Air kupasuka matairi wakati inatua kwenye
Uwanja wa Ndege wa Arusha leo mchana.
ARUSHA, Tanzania
ARUSHA, Tanzania
NDEGE ya kampuni ya Precision Air iliyokua ikitokea jijini Dar es salaam kuja mkoani Arusha hii leo imepata ajali baada ya magurudumu yake manne ya nyuma kupasuka wakati ikitua katika uwanja mdogo wa ndege wa Kilimo Anga Arusha.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa saba mchana lakini hakuna mtu yeyote aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo kwakua ilitua salama.
Alisema mpaka hivi sasa ndege hiyo ipo katika uwanja huo huku wataalamu mbalimbali wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini sababu ya ndege hiyo kupasuka magurudumu yake yote manne ya nyuma.
Hata hivyo kamanda Sabas alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa huwenda sababu kubwa ya kupasuka kwa magurudumu hayo ni kutokana na matope yaliyokuwepo katika njia ya kukimbilia ndege kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa.
Hata hivyo alisema kwa taarifa hizo za awali alizo nazo hajaweza kupata namba ya ndege hiyo iliyopata ajali kwakua alikua nje ya ofisi yake na kuahidi kuitolea ufafanuzi zaidi atakaporejea ofisini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269