Breaking News

Your Ad Spot

Dec 11, 2013

SAKATA LA ZITTO KABWE NA CHADEMA, MWANASHERIA WAKE KUKUTANA NA WAHARIRI ASUBUHI HII

MWANASHERIA wa Mbunge Zitto Zuberi Kabwe (Pichani), Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba,  Albert Msando, atazungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika Hoteli ya Serena leo tarehe 11/12/2013 kuanzia saa nne na nusu asubuhi.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge Zitto imesema dhima ya mkutano huo itakuwa kutoa ufafafunuzi juu  ya mashitaka 11 na majibu yake  ambayo  Zitto Kabwe  na washitakiwa wenzake walipewa na Kamati Kuu ya CHADEMA.

"Aidha, katika kikao hiki Ndugu Msando, kwa niaba ya wateja wake, ataeleza hatua ambazo wateja wake wanazichukua ndani ya chama katika kuhakikisha kwamba mgogoro uliopo unakwisha kwa amani na haraka iwezekanavyo bila kuleta athari zaidi kwa chama", imehitimisha taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages