Breaking News

Your Ad Spot

Jan 22, 2014

BRAVO YAPELEKA WENGINE WANNE KUFANYAKAZI DUBAI

Mbunge wa Temeke  Abbas Mtemvu leo amekabidhi tiketi na hati nyingine muhimu kwa vijana wanne wa Tanzania kwa ajili kuondoka leo kwenda Dubai, kufanya kazi za ajira kupitia Kampuni ya Bravo Job Centre Agency Ltd. Pichani Mtemvu akimkabidhi hati, mmoja wa vijana hao, Zainab Suleiman mkazi wa Buza Dar es Salaam, katika hafla iliyofanyika, jijini Dar es Salaam. Wengine wanaosubiri kupata hati hizo ni Zuhura Ismail mkazi wa Keko, Maimuna Ibrahim na Aziza Seleman wote wakazi wa Yombo. Wanaoshuhudia ni Maofisa kutoka Kampuni ya Bravo, Mohamed Said na Khalifa Mayamba.      Akizungumzia hatua hiyo ya kuwapeleka Vijana wa Kitanzania kwenda kufanya kazi Dubai, Mtemvu amesema, Wale wote waliokwishapelekwa huko  kupitia Kampuni ya Bravo, hakuna aliyepatwa na matatizo kidiplomasia au kudhalilishwa kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimeanza kuripoti.
     Mbunge huyo amesema, kutokana na Bravo kuhakikisha taratibu zote zinakuwa sahihi, wale wote waliokwishapelekwa huko wanaendelea vizuri.
    Amesema, kama wapo wanaopatwa na matatizo ya kidiplomasia au kunyanyaswa ni Vijana wanaopelekwa au kwenda huko kwa njia za panya.
    "Sisi tumekuwa tukizingatia taratibu zote, kwa hiyo si rahisi mtu tuliyempeleka huko akapata matatizo, yaliyo nje ya taratibu za ajira yake. Na hao wanaoandika kwamba waliopelekwa huko wanadhalilishwa basi hao hawatuhusu sisi, siyo waliopitia mikononi mwetu", alisema Mtemvu.

1 comment:

  1. Naomba unipatie contact za hiyo kampuni nami niombe kazi huko
    Pia naomba uniunganishe na Mh. Abass Mtemvu

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages