Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,
Dk. Kitila Mkumbo (pichani kulia) na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Mkoa wa
Arusha, Samson Mwigamba , wamevuliwa rasmi uanachama baada ya
kuhojiwa na Kikao cha Kamati ya Chadema kilichofanyika mjini Dar es Salaam.
Mbali ya Mwigamba na Dk. Kitila kuvuliwa uanachama kwa tuhuma za kuandika waraka wa siri wa mkakati wa mabadiliko ndani ya chama hicho, kitu ambacho kilionekana kama usaliti ndani ya chama hicho, Mtuhumiwa mwingine ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe ambaye suala lake linasubiri mpaka kesi aliyoifungua Mahakama Kuu itakapomalizika.
Kesi hiyo inaendelea tena leo katika Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salalaam.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Mbali ya Mwigamba na Dk. Kitila kuvuliwa uanachama kwa tuhuma za kuandika waraka wa siri wa mkakati wa mabadiliko ndani ya chama hicho, kitu ambacho kilionekana kama usaliti ndani ya chama hicho, Mtuhumiwa mwingine ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe ambaye suala lake linasubiri mpaka kesi aliyoifungua Mahakama Kuu itakapomalizika.
Kesi hiyo inaendelea tena leo katika Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salalaam.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269