Breaking News

Your Ad Spot

Jan 20, 2014

MBUNGE WA TEMEKE ABBAS MTEMVU AWAANDALIA CHAKULA CHA JIONI MARAFIKI ZAKE KATIKA MAENDELEO KUTOKA CHUO KIKUU CHA BUFFALO CHA NCHINI MAREKANI

Katika chakula cha jioni alichowaandalia marafiki zake katika maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Buffalo nchini Marehani, katika hoteli ya Sea Cliff nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu aliandaa cheki maalum ya urafiki kati ya Chuo hicho na Temeke.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) na Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Buffalo cha Marekani, Tyler Choi wakati wa hafla ya chakula cha usiki alichowaandalia marafiki zake hao  jana kwenye Hoteli ya Sea Cliff, Masaki Dar es Salaam.
Mtemvu (wa tatu kulia) akiwa na baadhi ya wageni kutoka Chuo Kikuu cha Buffalo Marekani wakipata mlo wa usiku. Ujumbe huo umepangiwa kuonana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na kutembelea baadhi ya shule na Hospitlai katika Jimbo la Temeke.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Ally (kushoto) na wenzie wakipata mlo huo
Mtemvu akidadiliana jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya African Maraika, Fiona Barrelto (katikati)  na mkewe Mariam wakati wa hafla hiyo.
Mfanyakazi wa Hoteli ya Sea Cliff (katikati) akichangamsha hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Sea Cliff wakiiimba wimbo huku wakipiga makofi ikiwa ni moja ya sham rashamra ya hafla hiyo.
Wageni ambao ni wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Buffalo Marekani wakiwa wamesiamama walipokuwa wakitambulishwa kwenye hafla hiyo.
Mtemvu akielezea umuhimu wa ziara ya marafiki zake hao nchini.
 Mwanafunzi Tyler Choi wa Chuo Kikuu ccha Bufalo akitoa shukurani kwa kuandaliwa hafla hiyo pamoja na kuahidi kudumisha urafiki uliopo na Mtemvu na Jimbo la Temeke kwa ujumla.
 Barrelto ambaye ni mfadhili mkubwa katika sekta ya elimu Jimbo la Temeke, akielezea umuhimu wa kudumisha urafiki uliopo kati ya chuo hicho na Mtemvu (kushoto). Kulia ni Mke wa Mtemvu, Mariam ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalum Temeke.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages