Breaking News

Your Ad Spot

Jan 16, 2014

PINDA AKAGUA MAAFA YA MAUAJI YA WAKULIMA KITETO

Eneo la Mtanzania  wilayani Kiteto  ambalo ni moja kati ya maeneo ya  makazi  yaliyovamiwa na watu wanaodaiwa kuwa wafugaji  ambapo watu watatu waliuawa na nyumba kuchomwa moto. Mlheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda alitembelea eneo hilo Januari  16, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanakijiji wa  Mtanzania Januari 16, 2013 wakati alipokwenda kuwapa pole  kufuatia uvamizi waliofanyiwa  na watu wanaosadikiwa kuwa wafugaji ambao waliua watu watatu  na kuchoma nyumba . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo.
Baadhi ya wananchi wa Kiteto  wakimsikiliza  Waziri Mkuu , Mizengo Pinda wakati alipowahutubia  Januari 16, 2014 katika mji wa Kibaya alipokwenda kuwapa pole wakulima wa wilaya hiyo  ambao walishambuliwa, kuuwawa na nyumba zao kuchomwa moto na  watu wanaosadikiwa kuwa  ni wafugaji.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Kiteto baada ya kuwasili wilayani humo  Januari 16, 2014  kufuatilia suala la mauaji ya wakulima
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na wazee  wa Kiteto wakati alipoteta nao baada ya kuhutubia  mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Kibaya Janauari 16, 2014. Alikwenda Kiteto kuwapa pole wakulima  ambao walishambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafugaji ambao waliua na  kuchoma moto nyumba.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na wazee  wa Kiteto wakati alipoteta nao baada ya kuhutubia  mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Kibaya Janauari 16, 2014. Alikwenda Kiteto kuwapa pole wakulima  ambao walishambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafugaji ambao waliua na  kuchoma moto nyumba. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages