Breaking News

Your Ad Spot

Jan 17, 2014

RAIS KIKWETE AMTEUA MHANDISI MASANJA KUWA KAMISHNA MPYA WA MADINI NCHINI

Rais Jakaya Kikwete amemteua Mhandisi Paul Mhangilwa Masanja kuwa Kamishna wa Madini nchini.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Obeni Y. Sefue mjini Dar Es Salaam leo, Ijumaa, Januari 17, 2014, na kusamabazwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini, imesema, uteuzi huo wa Injinia Masanja ulianza jana, Januari 16, 2014. Kabla ya uteuzi wake, Mhandisi Masanja alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages