VIKOSI
vya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa, vinamshikilia Edwin John Mponji
(31) kufuatia kwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga na kujitambulisha
kwamba yeye ni koplo wa jeshi la Wananchi JWTZ akitaka kijana wake
afanyiwe mpango wa kuingizwa Jeshi la kujenga Taifa.
'Koplo' Mponji
alikwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego Januari 16
mwaka huu siku ambayo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa ilikuwa
katika zoezi la kuwafanyia usaili vijana wanaotakiwa kujiunga na jeshi
la kujenga Taifa (JKT).
Akiwa
katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mponji alijitambulisha kuwa yeye ni
afisa wa JWTZ ambaye kwa sasa yupo kikosi cha 36 KJ Mkoani Pwani ambapo
aliambatana na kijana Emmanuel Joseph akitaka afanyiwe mpango ili apate
nafasi.
Hata
hivyo wakati akitoa maelezo hayo,Mshauri wa Mgambo wa Wilaya ya
Tanga,Sir Meja Albano Semfuko alimtilia shaka na kumjulisha Mkuu wa
Wilaya ambaye aliamuru ashikiliwe kwa mahojiano zaidi.
Akizungumza
na waandishi wa habari,Mkuu wa Wilaya ya Tanga alisema baada ya
mahojiano ilibainika kuwa Mponji sia askari wa JWTZ ndipo akalazimika
kupelekwa nyumbani kwake mtaa wa Magomeni Jijini hapa alipopekuliwa
alikutwa na sare za JWTZ zikiwa na cheo cha koplo.
Alisema
wakati akikamatwa,Mponji alikuwa amevaa kaptura ya jeshi la Polisi
lakini alipowekwa rumande ya kituo cha Polisi Chumbageni alifanya njama
za kuivua na kisha kumpa mahabusu aliyekuwa akitoka ambaye alitoweka
nayo.
Mponji
alionyeshwa kwa waandishi wa habari akiwa amevalia sare ya jeshi la
Wananchi ambapo alipohijiwa alishindwa kutoa maelezo ya kueleweka juu ya
wapi alikokuwa amezipata sare hizo inagawa alikiri kuwa aliwahi
kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kikosi cha 841 KJ Mafinga.
Kufuatia
tukio hilo,Mkuu wa Wilaya ya Tanga aliamuru Jeshi la Wananchi kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi kumfanyia uchunguzi wa kina ili kubaini
mtandao wake.
'Koplo' feki wa JWTZ akiwa ofisini kwa mkuu wa wilya.
'Koplo' feki akijiandaa kupanda kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi na chini ni
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269