KUAHIRISHA SAFARI YA TRENI
YA
ABIRIA KWENDA BARA HADI JUMAPILI JAN, 05, 2014
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia
abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa
kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni ya abiria iliyopangwa
kuondoka jana Ijumaa Januari 03, 2014
saa 3 usiku imeahirishwa hadi kesho
Jumapili Januari 05 , 2014, saa 3 usiku.
Taarifa imefafanua kuwa kutokana na mvua kunyesha mkoani Dodoma
na mikoa jirani eneo kati ya stesheni za
reli ya kati za Gulwe na Godegode zimejaa maji na kufunika njia ya reli mkesha
wa mwaka mpya wa 2014!.
Tokea juzi Januari 02, 2014 Wahandisi na mafundi wa kampuni za
TRL na Rahco kwenye sehemu husika wakifanya tathmini na kusimamia ukarabati wa maeneo mawili ya reli yaliyoharibika.
Kwa mujibu Mkururgenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo
Amani Kisamfu anayeongozwa kikosi kazi cha kukarabati amesema kazi ya ukarabati
inafanywa usiku na mchana kuona huduma zinaanza mapema iwezekanavyo ikiwemo huduma
ya usafiri wa treni za abiria uliopangwa kuanza tena hapo
kesho Jumapili Januari 05, 2014.
Kutokana na dharura hii treni za kutoka Mpanda, Kigoma na
Mwanza kuja Dar zimebadilishiwa muda na siku ya kuondoka hivyo basi, badala ya kuondoka jana Ijumaa Januari 03,
2014 sasa zitaondoka kesho Jumapili Januari 05, 2014 saa 2 asubuhi.
Aidha taarifa hii
iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa
TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza..
Imetolewa
na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Paschal
Mafikiri.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269