Breaking News

Your Ad Spot

Jan 2, 2014

ZITTO AMBWAGA TUNDULISU MAHAKAMA KUU, NI KATIKA OMBI LA KUPINGA ASIJADILIWE NA KAMATI KUU YA CHADEMA



 Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe (kulia) akitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam leo, ambapo aliwasilisha ombi la pingamizi la yeye kujadiliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinachotarajia kufanyika kesho, hadi rufaa yake ya kupinga kuenguliwa wadhifa huo kwenye Baraza Kuu la chama hicho. Kushoto ni Wakili wa Zitto, Albert Msando. Mahakama Kuu imekubaliana na Zitto Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kinachotarajiwa kufanyika kesho kutomjadili kwa namna yoyote.
                                Zitto Kabwe akiingia mahakama Kuu Dar es Salaam leo
 Wanasheria wa Chadema, Tundu Lisu (kushoto) na Peter Kibatala waliofika kupinga hoja hiyo mahakamani.
 Tundu Lisu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakijadiliana jambo wakati wakisubiri uamuzi wa mahakama
Zitto na wakili wake Msando wakiwasiliana na marafiki zao walipokuwa wakisubili uamuzi wa mahakama, ambapo Zitto aliibuka dedea kwa pingamizi lake kukubaliwa hivyo kikao cha Kamati Kuu kinachofanyika kesho kukatazwa kumjadili kwa namna yoyote Zitto.PICHA KWA HISANI YA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

1 comment:

  1. yetu macho, zzk komaa kama Mandela,,misukosuko ni kawaida ktk maisha,komaa nao hao wachaga,mara shibuda naye msaliti hawa vp? cwaelewi bhana wakina claha na mtu huru.

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages