Breaking News

Your Ad Spot

Jan 7, 2014

ZITTO KIDEDEA, AIBWAGA CHADEMA MBELE YA TUNDULISU MAHAKAMA KUU LEO

 HONGERA: Wakili wa CHADEMA Tundu Lisu (kulia) akilazimika kumpongeza aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe baada ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa, kuridhia zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya Chadema, hadi kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho itakapomalizika. Jaji huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza kusikilizwa Februari 13, mwaka huu.
 Zitto akitoka kwa msaada wa mabaunsa wake katika chumba cha mahakama kuu baada ya uamuzi huo wa  Mahakama kuu leo jioni.
Tundu Lisu na wapambe wake wakionekana kutoka kwa aibu Mahakamani baada ya kubwagwa
 Tundulisu aklizungumza na waandishi nje ya mahakama
 Wakili wa Zitto akizungumza na waandishi nje ya mahakama kuu
 Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto wakishangilia abaada ya ushindi wa kiongozi huyo
Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto wakiwa wamekaa chini kutii amri ya polisi baada ya matokeo ya kesi kutangazwa upende wao ukiwa aumeibuka kidedea
 Wafuasi wa Chadema wanaounga mkono uongozi wa chama hicho kutaka Zitto atimuliwe uanachama, wakiwa wameduwaa nje ya mahakama baada ya uamuzi wa Jaji, John
 Mmoja wa wafuasi wa Chadema upande wa wanaounga mkono uongozi akiwa amejeruhiwa kichwani baada ya kupigwa jiwe.
Mbwa mkali wa polisi akiwa tayari kwa lolote.
 Wafuasi wa Chadema wakivurumishana mawe Zitto alipowasili mahakamani
Wananchi wa kawaida wakilazimika kusalimia maisha yao kwa kutimua mbio baada ya wafuasi hao wa Chdema kuanza kuvurumishiana mawe Zitto alipowasili Mahakama kuu

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages