RAIS KIKWETE |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa
jana, Jumamosi, Februari 22, 2014, aliongoza harambee ya kupatikana kwa zaidi
ya sh milioni 600 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kisasa vya matibabu kwa
ajili ya Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, Dar Es Salaam.
Taaria iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam, imesema, katika
hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Dar Es Salaam, Rais
Kikwete pia ameahidi kuendeleza kuongoza jitihada za kupatikana kwa kiasi cha
sh milioni 328 ambazo zinahitaji kukamilisha hesabu ya sh. 929, 915,000 ambazo
ndizo zilikuwa lengo la halfa ya jana.
Halfa
hiyo pia iliwakutanisha viongozi wakuu wa awamu tatu za uongozi wa juu wa
Tanzania ambako Rais wa Pili wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Rais wa
Tatu za Tanzania, Mzee Benjamin William Mkapa walikuwa wenyeji wa halfa hiyo
kwa nyadhifa zao kama walezi wa Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania (PAT).
Uchangiaji
katika halfa hiyo ulikuwa wa aina tatu – kuna fedha taslimu milioni 55.4 zilizochangwa
moja kwa moja, kuna ahadi za uchangiaji na kuna wachangiaji walioamua kuwa
watatoa fedha za kununua vifaa mbali mbali vinavyohitajika katika Wodi hiyo
ambayo gharama yake inakadiriwa kufikia dola za Marekani 570,500.
Katika
halfa hiyo, Ikulu ya Rais Kikwete imetoa mchango wa kununua mashine iitwayo
Infant Radiant Warmer yenye thamani ya dola za Marekani 15,300 wakati Taasisi
ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayoongozwa na Mama Salma Kikwete imechangia
ununuzi wa mashine iitwayo Compressor Nebulizer ambayo gharama yake ni dola za
Marekani 12,000.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269