Breaking News

Your Ad Spot

Feb 23, 2014

SIMBA YALALA KWA MAAFANDE WA JKT RUVU

Dk 90+2..Musoti anapiga kichwa kinagonga mwamba Dk 90, Simba wanafanya shambulizi kali, Kiemba anapiga kipa anaokoa, Tambwe anapiga, kipa anaokoa, anaumia... sasa anatibiwa Dk 89, Kiemba anapiga shuti, kipa anadaka
Dk 87, Kiemba anapiha shuti mpira unagonga mwamba na kutoka nje GOOOOO Dk 84, krosi ya Kiemba, Tambwe anapiga kichwa, bao. Dk 82 Tambwe anapiga shuti lakini Dihile anaokoa Dk 79, Badru anashindwa kufunga yeye na kipa, Mgisa anaokoa
Dk 70, JKT wanamuingiza Salum Machaku kuchukua nafasi ya Bunu Dk 69 Damas Makwaya anapewa kadi nyekundu na kutoka nje ni baada ya kufanya faulo kwa makusudi.
Dk 68, Anatoka tena Awadhi anaingia Issa Rashid 'Baba Ubaya' GOOOOO Dk 65, Tambwe anafunga mkwaju huo
PENAAAT dk 64, Kiemba anaangushwa, mwamuzi anaweka penalti Dk 58, Badrua anapiga shuti lakini mabeki JKT wanaokoa

Dk 57, Tambwe anapiga kichwa vizuri lakini kinatoka nje kidogo GOOOOOO Dk 53, Emmanuel Swita anafunga bao la tatu kwa shuti kali baada ya kugongeana na Amosi Mgisa
dK 47, Badru anashindwa kufunga akiwa katika nafasi nzuri Dk 46, Anatoka Henry Joseph kaingia Uhuru Selemani.
HALF TIME GOOOOOO dK 45, Emmanuel Swita anapiga kifundi kabisa na kufunga

dK 44, Henru anamuangusha Amos Mgisa..PENAAAAT Dk 23, Kipa Juma Dihile anakaa muda mrefu na mpira, mwamuzi anapuliza faulo, Simba wanapiga lakini Jonas Mkude anapaisha juu...goal kick.

Dk 21, Kiemba anawatoka mabeki wa JKT, lakini pia anapiga shuti kuuubwa juu hadi mashabiki Simba wanazomea.

Dk 18, Tambwe anaingia ndani ya eneo la 18, yeye na kipa anapiga shuti kuuubwaa. Dk 16, Logarusic anamtoa Ndemla na nafasi yake inachukuliwa na Ally Badru. GOOOOO Dk 13, Hussein Bunu anapiga shuti na kufunga ikiwa ni baada ya kumchambua Henry Joseph.
Dk 7, Tambwe anaingia ndani ya eneo la hatari lakini anashindwa kufunga
Dk 4, Iddi Mbaga anapata nafasi ya kufunga lakini anapiga shuti dhaifu: Dodoo hizi ni kwa Mujibu wa salehjembe.com

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages