Sanya Juu ni mji mdogo ndani ya wilaya Siha Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni Km 25 toka Bomang'ombe na KM 50 toka Moshi Mjini, weekend hii nilifanikiwa kuutembelea Mji wa Sanya Juu ambapo siku ya Jumamosi mji huu huwa umechangamka kwa shamrashamra za kibiashara. katika pita pita zangu nilifanikiwa kulitembelea soko ila nilishangazwa na hali niliyo ikuta ya miundombinu isiyo kidhi na kulifanya soko kuonekana hatarishi kwawafanya biashara na wateja wao kiafya.
Huu ni msimu wa mvua kwa sehemu kubwa ya mkoa wa Kilimanjaro, hatua za haraka zinatakiwa kuchukuliwa kuimarisha miundombinu ya soko la Sanya Juu kuimarisha afya za wafanyabiashara na wateja wao.
|
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269