Breaking News

Your Ad Spot

Feb 8, 2014

TASWIRA YA MKUTANO WA NANE WA MWISHO KUHUSU MAENDELEO ENDELEVU BAADA YA 2015

Mkutano wa nane wa maajadiliano ya wazi kuhusu maandalizi ya malengo mpya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 (SDGs) umekamilika siku ya Ijumaa, Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Katika Mkutano huu wa wiki moja wajumbe walijadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu mada kadhaa ambazo ziliwasilishwa mbele yao kuangalia ni kwa namna gani zinaweza kuwa sehemu ya malengo hayo mapya ya maendeleo endelevu. Mada hizo zilihusu masuala ya Bahari, Misitu na Viumbe hai, Usawa wa Jinsia na uwezeshwaji wa wanawake, uzuiaji wa machafuko, uimarishaji wa amani, ujenzi wa amani baada ya machafuko, utawala wa sheria na utawala bora. Tanzania ni kati ya Mataifa 30 yaliyokuwa yamechaguliwa kuwa wajumbe wa majadiliano hayo ya wazi (Open Working Group), na imeshiriki kikamilifu tangu mkutano wa kwanza hadi wa mwisho. Pichani, Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, akizugumza katika mkutano huo wa mwisho wa maandalizi ya  malengo mapya ya maendeleo  endelevu baada ya 2015. Balozi Mushy ndiye aliyeongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo. Pembeni ni Noel Kaganda, Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mwisho wa maandalizi ya malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015
 Wajumbe wakifuatiali mchango wa Tanzania uliowasilishwa na  Balozi Mushy kuhusu  uzuiaji wa  machafuko,  uimarishaji wa amani, ujenzi wa amani baada ya machafuko, utawala wa sheria na utawala  bora.
 Wajumbe wakifuatiali mchango wa Tanzania uliowasilishwa na  Balozi Mushy kuhusu  uzuiaji wa  machafuko,  uimarishaji wa amani, ujenzi wa amani baada ya machafuko, utawala wa sheria na utawala  bora.
Wajumbe wakifuatiali mchango wa Tanzania uliowasilishwa na  Balozi Mushy kuhusu  uzuiaji wa  machafuko,  uimarishaji wa amani, ujenzi wa amani baada ya machafuko, utawala wa sheria na utawala  bora. Kwa taarifa zaidi kuhusu mchango wa Tanzania katika majadiliano hayo> BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages