Breaking News

Your Ad Spot

Mar 1, 2014

AJALI YA DALADALA NA VX ILIYOTOKEA KATIKA ENEO LA MWEKA, MOSHI VIJIJINI

Ajali imehusisha gari ya abiria aina ya hiace inayofanya safari zake kati ya Mweka na Moshi mjini  na Toyota Landcruiser VX iliyokuwa  imewabeba  wanafunzi wa Chuo Cha Usimamizi na Uhifadhi wa wanyama pori kilichopo Mweka , Moshi vijijini.

 Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo, Fred Mushi gari aina ya Toyota Landcruiser VX iligonga daladala  hiyo iliyo kuwa imesimama kupakia abiria kwenye kituo kimoja maarufu kwa jina la Kona. Ajali hiyo imetokea muda wa saa 10.30 jana jioni

Gari aina ya landcruiser VX iliyokuwa na wanafunzi toka chuo cha Mweka ikiwa imeharibika kutokana na kwenda kujikita kwenye mtaro wakati wa ajali hiyo.
Basi dogo la daladala ikiwa imeharibika baada ya ajali hilo. Taarifa za awali zimedai hali ya dereva ni  mbaya.PICHA NA HABARI NA mdau WITO MSAFIRI WA MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG





No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages