Na Chibura Makorongo, Kahama
Mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi
Majengo wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Said Joshua (12) amenusurika kufa baada
ya baba yake mzazi kujaribu kumchinja, kutokana na kile kinachodaiwa kuchoshwa na kumtibu
mtoto huyo maradhi ya muda mrefu..
Tukio hilo limetokea jana saa 11 alfajiri katika
kijiji cha Majengo, kata ya Majengo, tarafa ya Kahama mjini ambapo mwanamme
aitwaye Joshua Salvatory (37) mkazi wa Majengo,fundi baiskeli akiwa nyumbani
kwake alimkata kisu shingoni mtoto huyo na kuathiri koromeo lake.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya Kahama mkoni Shinyanga,Dkt Joseph
Fwoma alisema mtoto huyo alifikishwa hospitalini hapo baada ya kuokotwa na wasamaria
wema huku akivuja damu nyingi shingoni.
Dkt Fwoma alisema baada ya mtoto huyo kufikishwa
hospitalini madaktari walimfanyia upasuaji na kumshona sehemu ya koromeo
aliyochinjwa na hali yake inaendelea vizuri hasa baada ya kuongezwa damu.
Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo Mariamu Idd (35) alisema, mtoto wake alichukuliwa na baba yake mzazi siku moja kabla ya tukio na kwenda naye kwake eneo la Majengo mjini Kahama anakokaa.
“Nimepigiwa simu na kuelezwa taarifa za kuchinjwa kwa mwanangu na baada ya tukio baba wa mtoto amekimbilia kituo cha polisi Mjini Kahama kujisalimisha”,alieleza mama wa mtoto huyo.
“Baba wa mtoto huyu siku za nyuma,alikuwa akimchukua mwanangu mara kwa mara na kumpeleka nyumbani kwake,mimi nilishaachana naye, huwa anamrudisha,na amekuwa akidai kuchoshwa na huduma za matibabu kutokana na mtoto huyo kuwa na matatizo ya kiafya”,alifafanua mama huyo.

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha
kutokea kwa tukio hilo, ambapo, kamanda wa
polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla alisema chanzo cha tukio
hilo kinasadikiwa kuwa mtuhumiwa anaugua ugonjwa wa akili.
Wakati huo huo mtoto wa kiume (miezi 6) asiyefahamika
jina wala makazi yake amekutwa kichakani akiwa amefariki dunia na mwili wake
ukiwa hauna jeraha na ukiwa tayari umeanza kuharibika.
Kamanda Mangalla alisema tukio hilo limetokea Machi
4, mwaka huu saa 12 jioni katika kijiji na kata ya Mhongolo wilayani Kahama na
kuongeza kuwa inaonesha mtoto huyo alitupwa katika siku tatu zilizopita.
Alisema chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa huku
akiwataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi ili kumbaini na kumkamata
mtuhumiwa aliyetupa mtoto huyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269