Breaking News

Your Ad Spot

Mar 1, 2014

CCM YAENDELEZA MOTO WAKE WA KAMPENI ZA CHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA, LEO YARINDIMA KATA YA NZIHI

 Mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Godfrey Mgimwa (kushoto) akiwasalimia wananchi alipowasili kijiji cha Magubike kwa akili ya kunadi sera kwenye mkutano wa hadhara leo.
 Wananchi wakimbeba jujuu Mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, katika Kijiji cha Magubike katika Kata hiyo.
 Sahikamoo Mzee: Godfrey Mgimwa akimsalimia mmoja wa wazee wa kijiji cha Ilala Simba kata ya Nzihi, alipofika kuhutubia mkutano wa hadhara wa kuomba kura kwa wananchi wa kijiji hicho leo
 Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Salum Mtenga akimnadi mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa katika Kijiji cha Ilala Simba
 Kijana aliyehamasika katika Kijiji cha Magubika, akimsalimia kwa bashasha mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara
SISI HAPAAAA: Wananchi wa Kijiji cha Ilala Simba, katika Kata ya Nzihi wakinyoosha mikono, baada ya kuulizwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba nani kati yao mwenye kadi za kupiga kura ambaye atamchagua Mgimwa. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages