Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kombe la ushindi mwakilishi wa kampuni ya Jambo plastics Bi.Rupa Suchak baada ya kampuni yake kuibuka mshindi katika shindano la kuwania tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora wa mwaka 2013 katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku(picha na Freddy Maro)
BUNGE MAALUM LAPITISHA AZIMIO LA KURA YA MSETO
Na Magreth Kinabo – MAELEZO, Dodoma
Hatimaye baada ya mvutano wa baadhi wa wajumbe wa Bunge la Maalum la Katiba kuhusu upigaji wa kura ya siri na ya wazi kuendelea leo Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum, Mhe . Pandu Ameir Kificho amewasilisha azimio la mapendekezo ya ya upigaji kura wa wazi na siri kutumika kwa pamoja katika kaununi ya 37 na 38, ambalo limetipitishwa na Bunge hilo kwa matokeo ya jumla kwa kura ya ndiyo 376 na hapana 133 .
Kura hizo zimetangazwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge ,hilo, Mhe.Samia Sululu kabla ya kuahirisha kikao hicho leo usiku, ambapo alisema azimio hilo limepitishwa na Bunge hilo , kufuatia upigaji wa kura ,ambapo idadi ya kura zilizopigwa ni 509, wakati mauhudhurio ya wajumbe yalikuwa 511.
Mhe . Samia alisema kwa upande wa kura za wazi zilizopigwa ni 438, ambazo za ndiyo zilikuwa 351 na hapana ni 87, wakati kura za siri zilizopigwa zilikuwa ni 71, ambazo za ndiyo zilikuwa 25 na hapana ni 46.
Uamuzi huo umefuatiwa baada ya hali hiyo ambayo ilitokea tena kwa mara nyingine jana jioni mara baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum, Mhe . Kificho kuwasilisha mapendekezo ya upigaji kura wa wazi na siri kutumika kwa pamoja katika kaununi hizo.
Tangu jana jioni na leo baadhi ya wajumbe wamekuwa wakitoa michango kutaka upigaji kura huo uwe wa wazi na siri , huku wengine kutaka kura ya siri.
Awali Kanuni za 37 na 38 zilibaki kiporo tangu wakati wa utungaji wa kanuni mbalimbali za Bunge hilo, na uchangiaji wa kuziboresha, kutokana na mvutano huo, ambao baadhi ya wajumbe kutaka kura ya uwazi na wengine siri.
Wakizungumzia juu ya makubaliano yaliyofanywa na Kamati ndogo ya Muda ya Maridhiano na Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge kuhusu mapendekezo ya upigaji kura huo.
Mmoja ya wajumbe wa Kamati hiyo ndogo ya Maridhiano, John Nyika alisema walifanya mazungumzo hayo waliona ni vema wakubaliana mtu anayeweza kupiga kura ya uwazi na anayetaka ya siri wapige kulingana na matakwa yao ili kuwezesha mchakato huo kupiga hatua mbele.
“ Tunaomba utaratibu huu wa maridhiano uendelee … ili tuweze kupiga hatua mbele,” huku akisisitiza hawana dhamira yoyote ya kukwamisha mchakato wa Katiba mpya. Hivyo watakuwa wa kwanza kuunga mkono kwa kura azimio litakalopitishwa kwa kura zitakazokubaliwa.
Naye mjumbe mwingine wa kamati hiyo , Vuai Ali Vuai alisema jambo hilo ni kubwa kwa Watanzania ndio maana wanatakiwa kupiga kura kwa uwazi umma uweze kuona .
Kwa upande wake ,mjumbe mwingine wa kamati hiyo ya ndogo ya Maridhiano Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Donald Mtetemela amesema ni vizuri wajumbe hao wakakubali azimio hilo kwa kuwa mpaka sasa wameshatumia siku 40 kujadili kanuni za kuongoza Bunge hilo na zimetumia gharama hivyo wasiendelee kuongeza gharama, zipo siku tatu za kuomba ili kufanikisha maridhiano hayo.
“ Ninawaomba wajumbe wenzangu kukubali azimio hili ili tuweze kusonga mbele na na mchakato wa kupata Katiba ,” alisema Askofu Mtetemela.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269