Breaking News

Your Ad Spot

Mar 7, 2014

KAMPENI YA KUPAMBANA NA HOMA YA INI YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dk. Meshack Shimwela, akielezea madhara ya ugonjwa wa Homa ya Ini.
Shigongo akiwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kupambana dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Ini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akiandika huku akitafakari jambo wakati wa uzinduzi huo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe akielezea umuhimu wa wananchi kupima virusi vya ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B).
Meza kuu wakibadilishana mawazo.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakifuatilia uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akizindua rasmi kampeni ya kupambana na ugonjwa hatari wa Homa ya Ini.
Ini likiwa salama kabla ya kushambuliwa na virusi vya Hepatitis B.
...Ini baada ya kushambuliwa na virusi vya Hepatitis B.
...Ini lenye kansa.
Shigongo akimpongeza mgeni rasmi, Said Mecky Sadick baada ya uzinduzi.
Mmoja wa mapaparazi akijiandaa kuchukua matukio katika uzinduzi huo.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliofanikisha kampeni hiyo.
Mgeni rasmi akiagana na Eric Shigongo baada ya zoezi la uzinduzi kukamilika.
Wananchi wakipima virusi vya Hepatitis B vinavyosababisha ugonjwa wa Homa ya Ini.
Shigongo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari (DSJ) baada ya uzinduzi.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick amezindua rasmi kampeni ya kupambana na Ugonjwa wa Homa ya Ini katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam.
Kampeni hiyo imeandaliwa na Kampuni ya Global Pulishers Ltd wakishirikiana na Wizara ya Afya, SD Africa, Sanofi, Megra Clinic, Damu Salama na Tamsa.
Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewataka wadau mbalimbali kuonyesha ushirikiano katika kupambana na ugonjwa huo hatari kuliko HIV huku akiwaasa wananchi kuacha vitendo vinavyoweza kuleta maambukizi ya ugonjwa huo unaombukizwa kwa njia sawa na za HIV. (PICHA ZOTE NA GPL)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages