Na Flora kamaghe Iringa
Katibu wa
chama cha mapinduzi mkoa wa iringa Hassani
Mtenga amempa mda wa wiki moja Mkuu wa Kituo cha polisi mkoani Iringa
Siphaeli Pyuza kumuomba radhi kwa kitendo cha kwenda kufanya
oparesheni ndani ya jengo la Chama Cha Mapinduzi mkoa.
Mtenga (Pichani) alieleza
kuwa Pyuza alipita kila chumba bila ustaarabu wowote na kukagua kila chumba kwa
madai kuwa walipewa taarifa kuwa kuna
wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipigwa na kuteswa jambo ambalo Mtenga amesema halikuwa la ukweli
hivyo walienda kuwahukumu bila kuwa na uhakika wowote.
“tunatoa
masikitiko makubwa kwa ocd kuja kutupekua kila chumba ni kitendo cha
kutudhalilisha tunampa mda atuombe
radhi isiwe ni sehemu ya kuwasaidia Chadema”
Mbali na
hayo mtenga alitoa ufafanuzi juu ya
waraka uliovuja ambao Chadema walikuwa
nao kuwa ulikuwa na sahihi feki ya katibu mkuu mwigulu nchemba,waraka huo
ulikuwa ukitoa ufafanuzi juu ya fedha ambazo zimetolewa kwa Chama Cha Mapinduzi
kwaajili ya uchaguzi wa ubunge jimbo la kalenga.
Kwa madai ya
chadema walieleza kuwa fedha hizo zilionesha kuwa waalitumia rushwa kwa
wananchi ili kuweza kupata ushindi mkubwa wa jimbo la Kalenga kuweza
kuchukuliwa na Chama Cha Mapinduzi kwani barua waliokuwa nayo ilionesha matumizi ya fedha hizo lakini katibu
alikanusha suala hilo.
Hassan alieleza
kuwa hizo ni fitina tu za chama cha demokrasia na maendeleo ambazo wanatumia
kwaajili ya kuwachokonoa chama cha mapinduzi na alisema kuwa chadema wanapaswa
kuwa na akili kwani mambo wanayofanya ni kukidhalilisha chama chao
Hata hivyo Hassani
alisema kuwa CHADEMA wamekuwa wakimfuatilia kwa mda mrefu na aliwataka ugomvi wao wa kisiasa ufikie katika majukwaa
na sio kila kosa kukimbilia polisi
kwaajili ya kumtafutia mtu sababu ya kumkamata.
“Chadema
wanasema kuwa mimi nikikamatwa na polisi watafurahi sana wananitafutia mimi kosa
la kukamatwa kwasababu gani ugomvi wetu uishie majukwaani sio polis alisema
mtenga”
Hata hivyo Mtenga
amewataka wanachama wake kuendelea kuwa
na mshikamano na waweze kutekeleza ilani
ya chama cha mapinduzi na kuendelea kudumisha amani iliyopo katika nchi isiweze
kuvunjwa na mtu yeyote na endapo yeyote atakaekamatwa kushinikiza au kuvunja
amani hatua kali zitachukuliwa dhidi yake
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269