MKurugenzi wa Msama Promotions Ltd,ambao
ndio waandaji wa tamasha la krismass na Pasaka,Bwa.Alex Msama amesema kuwa
maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kuanza kufanyika jijini Dar
mnamo April,20 mwaka huu yamekamilika.
Aakizungumza na Waandishi wa habari jijini
dar leo katika viwanja vya Karimjee,Msama amebainisha kuwa kila kitu
kimekwishakamilika,wakiwemo wasanii mbalimbali watakaotumbuiza siku hiyo,aidha
amesema kuwa pamoja na wanamuziki wa nyumbani kushiriki tamasha hilo,pia
kutakuwepo na wanamuziki wengine kutoka nje ya nchi.
Msama amesema kuwa katika kuhakikisha
washabiki na watazamaji wanalifurahia tamasha hilo lenye kujaa nyimbo za
kumsifu na kumuabudu Mungu,kutakuwepo na wanamuziki nyota kutoka nchini Afrika
kusini,ambao watalipamba vyema tamasha hilo.
"Katika tamasha hilo kutakuwepo na
wanamuziki kutoka Afrika kusini,akiwemo Rebecca Malope mbaye atatumbuiza
kwenye hitimisho la tamasha hilo jijini Mwanza,pamoja na Mwanamuziki Kekeletso Phoofolo ambaye atatumbuiza hapa jijini Dar,wakiwemo na wanamuziki wengine wengi wa hapa
nyumbani kama vile Rose Muhando,Upendo Nkone,Bon Mwaitege,John Lisssu,Upendo
Kilahilo na wengineo wengi" alisema Msama.
Msama amesema kuwa Tamasha hilo litazunguka
mikoa isiyopungua tisa,ameongeza kuwa pia katika kuisadia jamii,Kamati ya
maandalizi ya tamasha la pasaka itaandaa fungu Maalum kwa ajili ya kuwapa
Mayatima na watoto waishio katika mazingira magumu.
Sisi kama Msama Promotions tutaandaa fungu
rasmi kwa ajili ya kusaidia watoto Yatima,lengo likiwa ni kuwapa fungu maalum
kwa ajili ya kujitegemea,mfano kuwaanzishia biashara ambayo itakuwa endelevu na
yenye kuwasaidia badala ya kupewa vitu vya kupita tu kila wakati"alisema
Msama.
Amesema kuwa watatoa fungu maalum kwa kila
kituo kwa kuwapa kiasi cha shilingi Milioni tano kwa kila kituo ili
kujiendeleza zaidi,na tunalitoa kutokana na mapato ya Pasaka,na mapato mengine
yatatumika kuendeleza ujenzi wa kituo cha watoto waishio katika mazingira
magumu ,Kituo cha Watoto kiitwacho Jakaya Mrisho Kikwete rafiki wa wasiojiweza.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269