Breaking News

Your Ad Spot

Mar 3, 2014

MALENGA WETU

NAMWOMBA KARIMA ANIPE LOLOTE  ISIPOKUWA  HILI TU
NaHemed Kivuyo (Sauti ya dhiki)
 Namshukuru KARIMA kwa yote anipayo pamoya nakuwa mengine yanaumiza tena yaumiza hasaa. Kuna Mambo yanatendeka huku chini ya jua yanaumiza sana. Binadamu tunatendeana mambo yasiyofaa.
 Aliwahi kuimba Nguli Marijani Rajabu. Si wanawake si wanaume. Marijani aliimba hayo miaka zaidi ya 20 iliyopita  seuze miaka hii!!!! ( MOLA AMLAZE PEMA)   Kuna mengi yaumizayo na yatokanayo na sisi sisi wanadamu. Lau kama bidamau mmoja tu angalikuwa anaishi peke yake ulimwenguni basi asingepata majeraha ya moyo yatokanayo na maudhi ya binadamu mwenzie. Tumeumbwa kuumizana??
Mwenyezimungu hawezi kutenda muujiza ( ingawa yeye ni mtenda yote) akanipaisha angani nikaishi mwenyewe ..la hasha!! RABUKA atanichukua siku moya kisha nitakwenda kujibu mbele yake yale yote niliyotenda ambayo yamekwenda kinyume na mafunzo yake hapa Duniani.
 ( MOLA NIEPUSHE) NAJUA mimi ni mkosefu tu mbele ya KARIMA , hivyo basi sina lolote la kujivunia na hata nikashindwa kukupenda na kukuheshimu wewe( unayesoma hapa) Nakupenda . Mwenyezi  Mungu Mwingi wa Rehma anaweza kunipa lolote atakalo. Nimekuwa nikiwaza na kuwazua bila majibu thabiti.
 Njua moyo ulivyokuwa dhaifu,najua  maudhui ya mwili wangu,najua moyo wangu unakiwango gani cha mapendo kwa nimpendaye. Kama siku moya ningalipewa nafasi nimshitakia KARIMA Kwa yale nisotaka anipe ,awali ningeanza na

hili..NINGEMWAMBIA KARIMA NAKUPENDA NA KUKUABUDU PAMOYA NA MTUME WAKE MUHHAMAD. NINGEWAMBIA KARIMA NAOMBA UNIPE LOLOTE UTAKALO ISIPOKUWA USINIPE MAPENZI..KARIMA USINIPE UGONJWA WA KUPENDA MTU KIMAPENZI. SITAKI KUPENDA MJA AITWAE MWANADAMU TENA WAKIKE..ABADAN..KARIMA NAKUOMBA SANA  NIPE LOLOTE LAKINI NIEPUSHE NA KUPENDA.

NILALAPO NAOMBA KARIMA ILI NIAMKE NA SIHA NJEMA NAHATA NDUGU NA JAMAA ZANGU,PIA NAOMBA USINIPE MARADHI YA KUPENDA DAIMA DAWAMA
.
NDUGU ZANGU MWAWEZA KUDHANI NIMEINGIWA MAJUNUNI LAKINI AAAHH. NI SALAMA NA SIHA NJEMA,NINA AKILI TIMAMU TENA NIKIZIAMINI. UGONJWA WA KUPENDA MIMI NIMESHINDWA KUUHIMILI. HIVYO SIONI SABABU YA KURUHUSU UGONJWA HUO KUNIINGIA INGAWA WAKATI MWNGINE  UGONJWA UNAINGIA PASIPO RIDHAA YANGU. NA NDIYOMANA NAMUOMBA RABUKA ASINIPE MAPENZI.CHAKULA HUKIONA SUMU, SI MAJI WALA  MURRDALI KITAKAOCHOINGIA KINYWANI..JAMANI SITAKI MAPENZI..NANYI MNIOMBEE KWA MOLA ASINIPE MARADHI HAYO…

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages