Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimnadi mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo
la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kwenye mkutano wa
kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Mazizi ambapo alisema moja ya sifa
za mgombea ni kuwafahamu wananchi wake, na wananchi wake kumfahamu,
kufahamu changamoto za wananchi na kufahamu namna ya kuzitatua
changamoto hizo.
Ridhiwani
Kikwete akijinadi kwa wananchi wa kijiji cha Mazizi kata ya Msata
ambapo aliahidi kujenga shule,kusaidia wakina mama na
vijana,kushirikiana na wana Chalinze katika kutafuta ufumbuzi wa
matatizo ya afya,kuinua kilimo,kufanya juhudi za dhati kuboresha kilimo.
Mjumbe wa Mkutano
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Ridhiwani Kikwete akifungua shina
la Tonga Road wakati wa ziara za mikutano ya kampeni za ubunge.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Tonga
wakati wa kumnadi mgombea wa CCM jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani
Kikwete.
Wazee wa kijiji
cha Diozile wakisoma vipeperushi vyenye wasifu wa Ridhiwani Kikwete
wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge jimbo la Chalinze zilizofanyika
kwenye viwanja vya shule ya msingi Lubaya.
Kila aina ya
furaha kwa vijana wa Msoga ambapo mgombea wa Ubunge jimbo la Chalinze
Ndugu Ridhiwani Kikwete alifanya mkutano wa hadhara kwa wananchi wa
kijiji hicho.
Karibu wa NEC
Itikadi na Uenezi akihutubia wapiga kura wa Ridhiwani Kikwete wakati wa
mkutano wa kampeni uliofanyika Msoga ambapo wananchi hao wamesema
kijijini kwao hakutokuwa na kura kwa wapinzani.
Mjumbe wa Mkutano
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Ridhiwani Kikwete akikata utepe kufungua shina
la UVCCM Msoga baada ya kumaliza mkutano wa hadhara wa kampeni za ubunge.
MGOMBEA UBUNGE KUPITIA CUF LAWAMANI CHALINZE
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akizungumza na Mwenyekiti
wa UWT Kata ya Ubena Jesca Daudi ambaye alivunjwa mkono na Viongozi wa
CUF waliovamia ofisi ya kata kwenye kijiji cha Tokamisasa.
Katibu
wa Wilaya ya Makete Miraji Mtaturu akizungumzia tukio lililomkuta
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Ubena Jesca Daudi ambaye alivunjwa mkono na
Viongozi wa CUF waliovamia ofisi ya kata kwenye kijiji cha Tokamisasa
kuwa ni kitendo cha kinyama na cha kupingwa kwa nguvu zote na kitendo
hicho kimemvua sifa za kuwa mgombea ubunge wa CUF.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269