Na Jovina
Bujulu
Suala la
Jinsia katika uongozi wa Bunge Maalum la Katiba limeibua Mjadala mzito katika nafasi
ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa bunge hilo.
Mjumbe wa
Bunge hilo Lediana Mung’ong’o ndiye aliyekuwa wa kwanza kuibua suala hilo
wakati wa mjadala kuhusu marekebisho ya kanuni za bunge kipengele 8(i)
kinachozungumzia utaratibu wa kumchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.
Mung’ong’o
alitaka kipengele hicho kuzingatia uhusiano wa kijinsia, ambapo kama mwenyekiti
atakuwa ni mwanaume, makamu wake awe mwanamke au kama Mwenyekiti atakuwa
mwanamke, makamu wake awe mwanaume.
“Mwenyekiti
hili suala la Mwenyekiti na Makamu wake hatuna budi kuangalia suala la jinsia
kwamba ikiwa mwenyekiti atakuwa ni mwanaume, makamu wake awe mwanamke au kama
Mwenyekiti atakuwa mwanamke, makamu wake awe mwanaume” alisema Mung’ong’o.
Naye Mjumbe
wa Bunge hilo Anna Abdalah alisema kuwa suala hilo lilikosewa Tangu awali hivyo
hakuna budi makubaliano yafanyike kwa busara maana wanawake wenye sifa na uwezo
wapo wengi Tanzania Bara na Zanzibar.
Akichangia katika
suala hilo Mjumbe wa Bunge Hilo ambaye ni Naibu Waziri Wizara ya Fedha Adam
Malima alisema kuwa ili kuwepo kwa amani na Mshikamano sheria haina budi kusema
wazi endapo Mwenyekiti atatoka Tanzania Bara basi Makamu wake atoke Zanzibar.
Akijibu hoja
hiyo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman alisema kuwa suala hilo liwe la marekebisho
lakini si kwa kuvunja sheria hiyo.
“Sharti
hilo likibadilishwa litakuwa ni kituko na tutakuwa tunarekebisha sheria ambazo
hazikutungwa na Bunge Maalum la Katiba hivyo ni busara kufanya makubaliano ili
kufikia muafaka wa jambo hilo" alisema
Othman Masoud Othman.
Othman Masoud Othman.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269