Breaking News

Your Ad Spot

Mar 29, 2014

WAKAZI WA KATA YA PERA WAAHIDI KURA NYINGI KWA RIDHIWANI KIKWETE, APRILI 6, MWAKA HUU.

CHALINZE, Tanzania

Wananchi wa Kata Pera katika jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani, wameahidi kumpa kura nyingia mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM,  Ridhiwani Kikwete, siku ya uchgaguzi mdogo wa jimbo hilo utakaofanyika Aprili 6, mwaka huu.
     Wakizungumza kwa nyakati tofauti jimboni hapa leo, wakananchi kadhaa wamesema, uamuzi wa kumpa kura nyingi Ridhiwani, umekuja kufuatia imani yao kwamba atatimiza ahadi ambazo amekuwa akitoa kwenye mikutano yake ya kampeni ambazo zinagusa kwa dhati changamoto zao kama elimu, maji, afyai na miundombinu ya  barabara jimboni humo.
   Pia wananchi hao wammeeleza kuridhika na ahadi ya mgombea huyo kuhusu namna  atakavyosaidia jamii ya wafugaji katika suala zima la kuongeza majosho ya mifugo na pia kutafuta suluhisho la kudumu la migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete  akihutubia wakazi wa kijiji cha Pera wakati wa mkutano wa kampeni za Ubunge Jimbo la Chalinze, Ridhiwani aliwaambia wananchi hao kura yao ya tarehe 6 mwezi wa Nne itakuwa ndio jibu la changamoto zote kwa wananchi wa jimbo la Chalinze kwani anatambua Changamoto zote za jimbo hilo.
 Imani Madega akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Pera na kuwataka wana CCM kuwa kitu kimoja na kuhakikisha Ridhiwani Kikwete anashinda kwa kura nyingi ilikufanikisha azma ya kusaidia jimbo la Chalinze kukua kimaendeleo inakua.
 Msanii Sam wa Ukweli akiruka juu na Morani wa Kimasai wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge kupitia CCM uliofanyika Mbala Kijiweni, kitongoji cha Mbala kwenye kijiji cha Chamakweza kata ya Pera .

 Meneja wa Kampeni za Ubunge CCM Jimbo la Chalinze Ndugu Steven Kazidi akizungumza na viongozi wa wafugaji wa kijiji cha  Chamakweza kata ya Pera wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Mbala Kijiweni.
 Mgombea Ubunge wa CCM Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wafugaji wa kijiji cha Chamakweza ,Ridhiwani alihutubia wafugaji hao ambao walimueleza kuwa wanatatizo kubwa la majosho ya mifugo yao na wanaamini yeye akiwa Mbunge atawasaidia katika kuboresha miundo mbinu itakayowasaidia kufuga kwa kisasa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages