Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Makamu wa Rais( Muungano) Samia Suluhu Hassan leo mjini Dodoma.
(PICHA NA
HASSAN SILAYO)
|
Na Jovina
Bujulu
Muungano wa
Tanzania umeendelea kuwa nyenzo na utambulisho muhimu katika kuleta umoja na
maendeleo katika taifa.
Hayo yamesemwa
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mh. Samia Suluhu Hassan
wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo mjini Dodoma.
“Miaka 50
ya Muungano imekuwa ni ya mafanikio makubwa ambayo yamewanufaisha wananchi
katika nyaja mbalimbali kijamii, kiuchumi, na Kisiasa” alisema Waziri Suluhu.
Waziri
Samia alisema kuwa muungano huo umeendelea kuwa kielelezo imara katika suala la
ulinzi na usalama hali iliyowezesha kuwepo kwa amani na utulivu nchini.
Katika suala
la haki za binadamu Waziri Samia alisema kuwa suala hilo limeendelea kupewa
kipaumbele ndani ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo wananchi wameendelea
kupata haki zao za msingi kupitia mahakama za Mwanzo hadi za Juu.
Akifafanua kuhusu
suala la elimu Waziri Samia alibainisha kuwa wanafunzi wenye sifa Tanzania Bara
na Zanzibar wanapatiwa mikopo ili kukidhi gharama za Masomo, hali iliyosabisha
uimarishwaji wa elimu ya juu kwani kuwekuwepo kwa ongezeko la vyuo vya elimu ya
juu kutoka 25 mwaka 2015 hadi 63 vilivyopo sasa.
Aidha
Waziri Samia alisema kuwa Serikali hizi mbili zinashirikiana katika kubuni na
kuibua miradi ya Maendeleo inayofadhiliwa na Serikali kwa Kushirikiana na
Wahisanai wa Maendeleo.
“Serikali
hizi zimekuwa na ushirikiano wa pamoja katika masuala ya mandeleo mfano Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii TASAF III, MACEMP, ASDPL na ASDP kwa ujumla imekuwa ni
chachu kubwa ya Maendeleo ya wananchi katika pande zote za Muungano” Alisema
Waziri Samia.
Waziri
Samia aliongeza kuwa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yalizinduliwa Zanzibar
tarehe 1 Machi na Rais wa Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein ambapo nembo ya
Muungano ilizinduliwa na sherehe za Muungano zitafanyika Dar es Salaam.
Kauli mbiu
ya Mwaka huu ni “Utanzania wetu ni Muungano wetu, Tuulinde, Tuumarishe na Kuudumisha.”
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269