Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika leo Chalinze.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari Chalinze, ambapo pamoja na kuwaambia tathmini ya CCM lakini aliwaambia kuhusu namna ambavyo vyama vingine havijakuwa kidemokrasia kiasi cha kuanza kubaguana hadi kwenye kampeni.
Mgombea wa CHADEMA Mathayo Torongey anayedaiwa kutelekezwa.
- Wabunge wagoma kuchangia kampeni Chalinze
- Washindwa kupeleka helkopta Chalinze
- Yadaiwa kisa ni ubaguzi walionao
Na Mwandishi Wetu,Chalinze
Torengei ametelekezwa na
Chadema kwasababu ya kabila lake na ukanda wake na ndio maana hata helkopta
wameshindwa kuipeleka ili kumsaidia kwenye kampeni.
Hayo yalisemwa jana na
Katibu na Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye wakati akitoa tathimini ya hali
ya kampeni za uchaguzi jimbo la Chalinze.
Alisema kuwa viongozi wa
Chadema wameonesha wazi kuwa hawana nia ya kumsaidia Torengei na sababu kubwa
ni moja tu kuwa si mwenzao.
" Wabunge wa
Chadema wamekuwa na utamaduni wa kuchanga fedha zinapotokea chaguzi lakini kwa
huyu mgombea wao wa Chalinze wamegoma kufanya hivyo.
"Wamekuwa wakifanya
ubaguzi lakini sasa ni dhahiri kuwa wameonesha kile ambacho kipo moyoni mwao.
"Ukifanya uchunguzi
utabaini hakuna mahali ambapo Chadema hawakutumia helkopta katika uchaguzi
mdogo ambapo walishawahi kutumia helikopta kwa uchaguzi wa Udiwani tu Arusha.
Alifafanua kuwa Torongei
ametapeliwa na Chadema na hilo litakuwa fundisho kubwa kwake na kwamba
ameingizwa mkenge.
"Anachotakiwa kujua
jamaa hao ni matapeli na ameingizwa mkenge.Tunajua baada ya uchaguzi huu si
atashindwa kupata kura bali atakuwa amefilisika,"alisema Nape.
Aliongeza kutokana na
kumsusia uchaguzi huo, hata vijana ambao wameletwa na Chadema kwa ajili ya
kufanya vurugu wanaishi maisha ya kuomba omba.
"Wamewaleta vijana
lakini nao wanaishi maisha ya kubahatisha.Wamefikia mahali vijana wao wanakuja
kuomba fedha ya kula tunawapa.
"Hivyo kama wao nao
wameishiwa wasione aibu maana kitendo cha kumsusa mgombea wao, wachache waliopo
wanaishi maisha magumu sana,"alisema Nape.
Akizungumzia ushindi wa
chama hicho, Nape alisema kwa hali ilivyo watashinda kwa zaidi ya asilimia 94.
"Ushindi wetu
katika uchaguzi unaotarajia kufanyika Aprili 6 ambayo itakuwa Jumapili ni zaidi
ya asilimia hizo.Wapinzani hawana lolote na watashindwa vibaya kuliko
wanavyotarajia,"alisema.
Kuhusu kampeni
zinazoendelea, alisema zinakwenda vizuri lakini wapinzani hasa Chadema
wanafanya hujma za kuiba shahada za kupigia kura kupitia watoto ambao wanawapa
fedha ili waziibe kwa wazazi.
"Tunazo taarifa
kuwa kuna baadhi ya maeneo wananchi wanalalamika Chadema wanatumia watoto kuiba
shahada hizo kwa lengo la kupunguza ushindi wa CCM pia kutoa taarifa za uwongo
kuhusu tarehe ya kupiga kura kwa kuwaaminisha wapiga kura kuwa uchaguzi utakuwa
mwezi wa sita tarehe 6,"alisema Nape.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269