Breaking News

Your Ad Spot

Apr 15, 2014

ZIARA YA KATAVI YAMFIKISHA KINANA NYUMBANI KWA WAZAZI WA PINDA, KIBAONI LEO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mama mzazi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Bibi, Zenita Mkaawima, alipotembelea nyumbani kwa Wazazi wa waziri Mkuu huyo, Kijiji cha Kibaoni, wilayani Mlele mkoani Katavi, leo
 Mdogo wa Waziri Mkuu Mizengo Pinga, Wofgaga Pinda, akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, alipowasili nyumbani kwa wazazi wa Waziri Mkuu, katika kijiji cha Kibaoni, mkoani Katavi. 
 Kinana akiwa katika mazungumzo na Mama wa Waziri Mkuu, na mdogo wa waziri huyo mkuu, leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
 Kinana na Nape na Balozi Ali Karume (wapili kulia) wakiwa  katika picha ya pamoja na mama mzazi wa Waziri Mkuu, wakiwa katika picha ya pamoja nyumbani kwa Mama huyo, Kibaoni mkoani Katavi.
 Kinana akiagana na mama wa waziri
 Nape akimfurahia mtoto aliyemtania kwa jina la Pinda, yeye na Kinana walipotembelea nyumbani kwa wazazi wa Waziri Mkuu Mizengo pinda leo

 Kinana akikagua tanki la mradi wa maji wa  Kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi
Kinana akikagua ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Kibaoni wilayani Mulele, Katavi
 Kinana akiwa katika shamba la ufuta la Waziri Mkuu, Pinda lililopo katika Kijiji cha Kibaoni, alikozaliwa waziri mkuu huyo
 Kinana akiwatuza wasanii waliotumbuiza baada ya kuwasili katika kijiji cha Kibaoni

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua mashine ya kukoboa mpunga katika Kijiji cha Mwamapuli, Kata ya Majimoto, mkoani Katavi
 Nape akishiriki ujenzi wa shule ya msingi Majimoto, leo
 Kinana akishirikiana na wananchi wengine kusogeza matofali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Majimoto mkoani Katavi
Katibu Mkuu wa CCM Abdulahman Kinana akibeba zege wakati akishiriki ujenzi wa shule ya Majimoto
 Kinana akiwa amevishwa mgolole na kupewa silaha za jadi alipotawazwa na wazee wa Kisukuma kuwa mmoja wa wazee wa kabila hilo wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Majimoto, wilayani Mulele.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara, katika Kijiji cha Mlele, leo
Kinana akishiriki kucheza ngoma ya jadi ya wasukuma baada ya mkutano huo. Picha zote na Bashir Nkoromo- theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages