Breaking News

Your Ad Spot

Apr 4, 2014

ZIARA YA KINANA SUMBAWANGA MJINI, ASIKILIZA KERO ZA WAFANYABIASHARA, MAELFU WAFURIKA MKUTANO WAKE KIJIJI CHA MAWENZUZI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Sumbawanga mjini, Hilary Aeshi wakisalimia wananchi, Kinana aliopowasili kwenye Kijiji cha Mawenzuzi, kuhutubia mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na kusikiliza kero za wananchi katika wilaya ya Sumbawanga mjini leo

 Kinana akizindua shina la wakereketwa wa CCM kijiji cha Mawenzuzi wakati wa ziara hiyo
 Mbunge wa Sumbawanga mjini Hilary Aeshi akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati wa uzinduzi wa shina hilo.

 Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Kijiji cha Mawenzuzi, Sumbawanga mjini leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyabiashara wa Mji wa Sumbawanga, kuhusu matatizo mbalimbali ikiwemo utitiri wa kodi na jinsi wanavyosumbuliwa  na maofisa biashara pamoja na malalamiko yao kuhusu mashine za TRA.Mazungumzo hayo yalifanyika leo katika Jengo la Chama cha Walimu, mjini Sumbawanga.
Wafanyabiashara wakiwa kwenye mkutano huo na Kinana Kinana
MfanyabiasharaWillington Kiziba  akilalamika mbele ya Kinana kuhusu kodi nyingi za biasshara na mazao ya kilimo.
Mfanyabiashara Nobert Mbala akielezea mbele ya Kinana jinsi wanfanyabiashara wanavyonyaswa
 Honory Daud naye akielezea jinsi wanyabishara wanavyonyanyaswa kiasi cha kuichukia Serikali  
Mfanyabiashara Martine Tulo akilalamikia kitendo cha Manispaa kuweka kodi ya Fire wakati wa ununuzi wa viwanja

Meya wa Manispaa ya Sumbawanga, Sabas Katepa akikiri mbele ya Kinana na wafanyabiashara kuhusu mpangilio mbovu wa kodi na malipo ya leseni na kuahidi kuyafanyia maboresho haraka
 Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, naye akikiri mbele ya Kinana kutowashirikisha wafanyabiashara kupanga kodi mbalimbali
Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aeshi akikubali kuwepo matatizo hayo na kuahidi kusaidiana na Kinana kupata ufumbuzi wa kero hizo ikiwemo ya mashine za TRA
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini, Emmanuel Kilindu  akitembelea magongo alipokuwa akitoka kwenye mkutano  na wafanyabiashara
Kinana (wa pili kuliai)akiwa na maofisa wengine wa CCM wakitoka kwenye mkutano na wafanyabiashara wa Mji wa Sumbawanga.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages