Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band mwanamuziki mpiganaji
aleyepachikwa majina mengi ya utani kutokana na matukio
Unapoutaja muziki wa dansi wa Tannzania maarufu kama "Bongo Dansi" jina la
Mwamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja na mzimu wake
"Ngoma Africa band" aka FFU-Ughaibuni ukipenda waite "Watoto wa Mbwa"
au Viumbe wa ajabu "Anunnaki Elien" yenye makao yake kule Ujerumani.
Mwanamuziki
Kamanda Ras Makunja wa FFU-Ughaibuni,tunamtaja kuwa Mpiganaji na mmoja
wa watunzi wachache sana wa muziki dansi ambaye nyimbo au tungo zake
zina uzito na ujumbe mkubwa kwa jamii,na maana nyingine nyimbo zake
zinamafunzo fulani,pamoja na sifa hizo mwanamuziki huyu Kamnada Ras
Makunja na mzimu wake "Ngoma Africa Band" ukimsikiliza sana utagundua
kuwa ujumbe ulio katika nyimbo zake mara nyingine haumezeki rohoni, kwa
jinsi unavyolenga au kuzungumzia kero fulani katika jamii ,kwa tabia
hizi yeye na bendi yake wamejikuta wakiitwa "Watoto wa Mbwa" yaani wasione kitu lazima watabwaka !
Mara
nyingine Mtunzi huyu Kamanda Ras Makunja aliyeipindia akili kazi
yake,anapoona nyimbo zake zimekuwa cheche za moto uwa anapooza kwa
kupeleka ujumbe mzuri kwa jamii wenye kuziteka nyoyo za wengi na kuweza kuzipiga masaji roho za walio wengi "Bongo Tambarare" hapo kamanda Ras Makunja na kikosi chake Ngoma Africa Band wanaonekana kuwa watoto wazuri lakini tabia zao ni kama ngozi hazibadiriki wawapo jukwaani ni sawa na askari wa kutuliza ghasia FFU,
kwa sababu wanajua wazi tabia za washabiki wao za kupenda mdundo live
wenye kasi kubwa kwa mtindo huu wamefanikiwa kuteka mamilioni ya
washabiki nje na ndani ya ughaibuni.
Ras Makunja na Muzimu wake "Ngoma Africa Band" wapo ndani ya medani
ya muziki wa dansi takribani miaka 21 na kushika chati katika majukwaa
ya kimataifa. inasemekana Ngoma Africa band ina himaya yake inayoitwa "Anunnaki Empire" himaya
ya viumbe wa ajabu (wasanii na waliowazunguka) katika makao ya
bendi,wakiwemo mafundi mitambo ambao kazi yao ni kuhakikisha kila kitu
kinacho fanywa ni " Extraordinary" mpaka mziki wenyewe ni "Extraordinary Bongo Dansi" himaya yao haina uwoga bali inatishia wapinzani wao.
Mwanamuziki Ras Makunja inasemekana hatumii ulevi wa aina yoyote hile wa
kuvuta sigara au kasumba bali ni mtu wa mazoezi makali ya kimwili na kihisia,
mazoezi ambayo watu wengi wanadai kuwa yanamsaidia kuongoza kikosi chake
anaposafiri
na kufanya tour ndefu,pengine katika nchi zenye utamaduni tofauti na wa
afrika. Kamanda Ras Makunja kufanya nae kazi inabidi uwe mjeshi sio
mchezo,kwa sababu hana mdhaa katika kibarua chake.
hivi karibuni inasemekana amesharekodi kibao kipya kinachoitwa " Myonge Mnyongeni ! Haki yake Mpeni" wimbo ambao utatolewa baadaye.
Muziki wa bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya unasikika pia katika tuvoti atwww.ngoma-africa.com pia www.reverbnation.com/ ngomaafricaband
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269