Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanda jukwaani, kuhutubia mkutano wa hadhara mwishoni mwa ziara yake ya siku moja katika wilaya mpya ya Kaliua mkoani Tabora, leo Jumamosi, Mei 17, 2014,
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji mdogo wa Kaliua akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia za kuzitatu mkoani tabora. Katika hotuba yake pamoja na mambo mengine ameahidi kuhakikisha tatizo la wakulima wa tumbaku la kizungumkuti katika kuuza zao hilo baina yao na vyama vya ushirika kupata ufumbuzi wa kudumu,
Wananchi wakimshangilia Kinana kwenye mkutano huo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye mkutano huo. Nape amewataka wananchi kuwa macho dhidi ya vyama vya siasa kupigana vikumbo kutaka idadi ya serikali kadhaa wa kadhaa katika mchakato wa Katiba mpya badala ya kupigania katiba yenye maslahi ya wananchi. Nape amesema, wanaopigania kuhusu idadi ya serikali ni watafuta madaraka tu na kwamba CCM haihitaji Katiba yeneye mlengo huo bali inahitaji Katiba itakayoweka mbele maslahi ya wananchi kwa kusukuma mbele maendeleo yao.
Mbunge wa Kaliua, Profesa Juma Kapuya akieleza alivyosimamia utekelezaji wa ilani ya Chama katika jimbo hilo.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana, akishauriana jambo na Mkuu wa mkoa wa tabora Fatma Mwasa na Katibu wa NEC Itrikadi na Uenezi Nape wakati wa mkutano huo.
Nape akimsikiliza kwa makini Fatma Mwasa alipokuwa akimweleza jambo ambalo linaelekea kuwa lilikuwa la ushauri mkubwa kwa maslahi ya Chama na Serikali ya CCM, wakati wa mkutano huo
Mtayarishaji Mkuu wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo (kulia) akiwa na wadau Octavian Kimario na Nyakia kwenye mkutano huo. (Picha zote na Bashir Nkoromo- thNkoromo Blog
Your Ad Spot
May 17, 2014
Home
Unlabelled
KINANA AMALIZA ZIARA URAMBO AKIAHIDI KUPATIKANA DAWA YA KUDUMU YA TATIZO LA WAKULIMA WA PAMBA
KINANA AMALIZA ZIARA URAMBO AKIAHIDI KUPATIKANA DAWA YA KUDUMU YA TATIZO LA WAKULIMA WA PAMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269