Breaking News

Your Ad Spot

May 2, 2014

MAKAMU WA RAIS DR.MOHAMED GHALIB BILALI AWASHA MWENGE MKOANI KAGERA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera leo Mei 2, 2014. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda, baada ya kuuwasha rasmi wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabian Masawe, akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Rachel Kasanda.
Vijana wenye dhamana ya kukimbiza mwenge wa Uhuru 2014, wakianza rasmi mbio hizo baada ya kuwashwa na kukabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa Sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge huo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba Mkoa wa Kagera leo Mei 2, 2014. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages