Watafiti wa Marekani wamebaini miili ya watoto hao hutoa viini vya kinga ambavyo hushambulia wadudu wanaosababisha Malaria.
Kwa kumdunga mtu sindano yenye viini hivyo vyo mtu anaweza kukingwa na ugonjwa huo .
Watafiti
hao ambao walichapisha matokeo yao kwenye jarida la kisayansi ,
wanasema majaribio ya utafiti huo katika binadamu na katika sokwe sasa
yanahitaji kutathminiwa kikamilifu ili kupata matumaini halisi ya chanjo
ya malaria.
Prof
Jake Kurtis, mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa afya wa kimataifa katika
hospitali ya kisiwa cha Rhode katika chuo kikuu cha tiba cha Brown ,
alisema : "Nadhani kuna ushahidi wa kuaminika kwamba hii inaashiria
upattikanaji wa chanjo ''
" Hata
hivyo wadudu wa malaria ni vigumu kuwashambulia'' . Kwa kweli ni maadui
wakubwa ." aliongeza Kurtis. Utafiti huo ulianza kwa kundi la watoto wa
shule 1000 nchini Tanzania , ambao sampuli za damu yao zilichunguzwa
mara kwa mara katika miaka ya mwanzo ya maisha yao .
Asilimia
6 ya watoto ya watoto hawa waliweza kuwa na kinga asilia kwa malaria,
licha ya kuishi katika eneo ambako ugonjwa huo umekithiri.Chanzo BBC
Swahili
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269