Mechi
ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini
Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe iliyochezwa Jumapili
katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 63,345,000.
Mapato
hayo katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Taifa Stars kuibuka na ushindi
wa bao 1-0 yametokana na washabiki 11,079 waliokata tiketi kushuhudia
pambano hilo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000.
Mgawo
wa mapato hayo ni asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
ambayo ni sh. 9,662,796.61, gharama za kuchapa tiketi sh. 6,000,000,
asilimia 15 ya uwanja ni sh. 7,152,330.51, asilimia 20 ya gharama za
mchezo sh. 9,536,440.68 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa pamoja wamepata sh.
30,993,432.20.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269