Bi
Regina Gwae ( wapili kushoto), Akiongea na wana habari kwa niaba ya
kamati ya maandalizi ya Nice and lovely jijini Dar es Salaam kuhusu
shindano la miss Tanga linalo tarajiwa kufanyika tarehe 21 juni 2014
katika ukumbi wa Mkonge hotel (watatu kulia),Meneja Mauzo Nice and
lovely Bw.Brian Kelly.
waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
Bi
Regina Gwae (kushoto),akiwaonyesha waandishi wa habari gari lenye
thamani ya shilingi miliono 10 toka kwa kampuni ya Nice and lovely litakalo shindaniwa katika shindano hilo (kulia), meneja mauzo wa kampuni hiyo Bw.Brian Kelly.
======== ==== ======
Wito
umetolewa kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga na vitongoji vyake kujitokeza kwa
wingi kushuhudia shindano kubwa na la aina yake la kuwania taji la
ulimbwende linalo tarajiwa kufanyika tarehe 21 juni 2014 katika ukumbi
wa Mkonge hotel.
Akiongea
na wana habari kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya Nice and lovely Bi
Rejina Gwae amesema kuwa wanajivunia kupata nafasi ya kuwa waandaji wa
shindano hilo na kutoa wito kwa warembo wote wenye nia ya kushiriki
kujitokeza kwa wingi.
Kuhusu
zawadi kwa mshindi Bi Rejina amesema kuwa mshindi ataondoka na gari
lenye thamani ya shilingi miliono 10 toka kwa kampuni ya Nice and lovely
akasema kuwa pia kuna zawadi nyingine za pesa taslimu toka kwa washindi
wengine ambazo wanatarajia kuzitangaza baadae.
Kwa
upande wake meneja mauzo wa Loreal wamilikiwa wa bidhaa za Nice and
lovely Briyan Kelly alianza kwa kuishukuru kampuni ya Mac D promotion
kwa kuwapa nafasi ya kuwa wadhamini wa nafasi hiyo na kuahidi kuitendea
haki nafasi hiyo.
Akamalizia
kwa kutoa wito kwa wote wenye nia ya kushiriki katika shindano hilo
kujitokeza kwa wingi na kusema kuwa fomu za kushiriki zinapatikana
Mkonge hotel, D,boutique tanga mjini,Breez fm,Tanga beach resort, Five
brothers, Mwambao fm, Sophia records, Danny fashion barabara ya 13,
ofisi za the guardian tanga barabara ya 15 na Yolanda salon mtaa wa
Eckenford na Nyumbani hotel.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269