Breaking News

Your Ad Spot

May 30, 2014

Picha na Taarifa:Jeshi la Magereza nchini kupitia Shirika lake la uzalishaji mali (Prisons Corporation Sole) limetiliana Mkataba wa uwekezaji na Mfuko wa Jamii wa GEPF ambapo majengo ya vitega uchumi yatajengwa katika maeneo ya Kihonda Mkoani Morogoro na Karanga Moshi Mkoani Kilimanjaro.


Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) na Bw. Daud Msangi   Mkurugenzi Mkuu wa GEPF (kulia) wakisaini Mkataba wa Uwekezaji baina ya Taasisi hizo mbili leo Alhamis 29 Mei, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Shirika la Magereza ( Prisons Corporation Sole) Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) John Masunga (kushoto) pamoja na Mwanasheria wa GEPF Anna Shayo (kulia) wakisaini nyaraka muhimu za makubaliano ya uwezekaji kati ya Magereza na GEPF).
 Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) na Bw. Daud Msangi   Mkurugenzi Mkuu wa GEPF (kulia) wakikabidhiana nyaraka za makubaliano ya uwekezaji baada ya kutiwa sahini.leo Alhamis 29 Mei, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Jijini Dar es salaam

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages