Breaking News

Your Ad Spot

May 23, 2014

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MAJI, YAZINDUA MWONGOWA UTENDAJI KWA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI.

 Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Injinia Mbogo Mfutakamba (katikati) wakati wa akizindua chapisho la Kanuni na utaratibu wa kuzingatia kwa Mamlaka zinazohusika na usimamizi  na usambazaji wa maji nchini wakati wa mkutano wa mwaka wa wataalaam na watendaji wa usimamizi wa sekta ya maji nchini. 
 Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Injinia Mbogo Mfutakamba (katikati) akiwaonesha wataalam na watendaji wa  usimamizi wa sekta ya maji nchini chapisho la Kanuni na utaratibu wa kuzingatia kwa Mamlaka zinazohusika na usimamizi  na usambazaji wa maji nchini wakati wa mkutano wao wa mwaka jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Uwezeshaji wa Maendeleo ya Miradi ya Maji kutoka shirika la GIZ nchini Dkt. Fred Lerise akitoa ufafanuzi kwa wataalam wa maji  kuhusu  chapisho la Kanuni na utaratibu wa kuzingatia kwa Mamlaka zinazohusika na usimamizi  na usambazaji wa maji nchini wakati wa mkutano huo wa mafunzo wa mwaka uliowahusisha wataalam na watendaji wa mamlaka za maji kutoka maeneo mbalimbali nchini. 
 Mtendaji JPIwa Shirikisho la Wasambazaji wa Maji nchini (ATAWAS) Bi. Martha Kabuzya akizungumzia umuhimu wa chapisho hilo kwa sekta ya maji nchini na kutoa wito kwa mamlaka zote nchini kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuhakikisha kuwa wateja wanaowahudumia wanapata huduma bora.
 Sehemu ya Wataalam nawatendaji wa Mamlaka zinazohusika na usimamizi  na usambazaji wa maji nchini waliohudhuria mkutano wa mwaka wa wataalaam na watendaji wa usimamizi wa sekta ya maji nchini. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
 
 Meneja wa Mamlaka ya Maji wilaya ya Mkuranga Injinia Filbert Pius (kushoto) akipokea  chapisho la Kanuni na utaratibu wa kuzingatia kwa Mamlaka zinazohusika na usimamizi  na usambazaji wa maji nchini kutoka kwa Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Injinia Mbogo Mfutakamba wakati wa mkutano wa mafunzo wa mwaka uliowahusisha wataalam na watendaji wa mamlaka za maji kutoka maeneo mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages