JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UPOTOSHWAJI WA UGONJWA WA HOMA YA DENGUE.
Wizara ya Afya na
Ustawi wa jamii inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa mbalimbali za
upotoshaji unaofanywa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii, simu za mikononi
na mikusanyiko ya watu kuwa ugonjwa wa Dengue haupo nchini Tanzania.
Wizara inapenda
kusisitiza kwamba, ugonjwa huo upo nchini na serikali kwa kushirikiana na
wananchi inaendelea kutekeleza hatua mbalimbali za kukabiliana nao. Ikumbukwe
ugonjwa huu unapatikana pia katika nchi nyingi duniani zilizoko katika ukanda
wa joto na unaathiri takribani asilimia 40 ya watu duniani.Takwimu za Shirika
la Afya Duniani zinathibitisha kuwa takribani watu milioni 5 wanaripotiwa
kuugua ugonjwa wa kila mwaka.
Wizara inasisitiza na kuikumbusha
jamii kwamba hakuna dawa maalumu ya ugonjwa wala chanjo bali mgonjwa anatibiwa
kutokana na dalili zitakazo ambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa
maji au damu.
Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya Dengue
o
Kuangamiza mazalio ya mbu
ü
Fukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia viuatilifu vya kuua viluwiluwi
vya mbu kwenye madimbwi hayo
ü
Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile:
vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.
ü
Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
ü
Hakikisha maua yanayo pandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu
maji kutuama
ü
Funika mashimo ya maji taka
kwa mfuniko imara
ü
Safisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama
o
Kujikinga na kuumwa na mbu
ü
Tumia viuatilifu
vya kufukuza mbu “mosquito repellants”
ü
Vaa nguo ndefu kujikinga na kuumwa na mbu
ü
Tumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu (kwa wale
wanaolala majira ya mchana na hasa kwa watoto)
ü
Weka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi
Wizara inawakumbusha wananchi wa
Tanzania kuwa, huu ni muda muafaka wa kuzingatia utunzaji bora wa mazingira
yetu. Tukitunza mazingira yetu, nayo yatatutunza na kutuepusha na maradhi
yanayoambatana na mazingira machafu.
Nsachris Mwamwaja
Msemaji wa wizara
23 mei 2014
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269