Breaking News

Your Ad Spot

May 30, 2014

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA ZAHANATI YA TABATA NBC‏

 Ofisa Uhusiano Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kisima kilichojengwa kwa msaada wa kampuni hiyo katika Zahanati ya NBC Tabata, Dar es Salaam. Kisima hicho kilizinduliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Ilala, Angelina Malembeka. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Ilala, Willy Sangu na anayefuatia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dk Assenga Severine na kulia ni Mganga Mfawidhi Zahanati ya Tabata NBC, Catherine Akili.
 Wauguzi wa Zahanati ya Tabata NBC, Dar es Salaam, wakishangilia baada ya Ofisa Uhusiano Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu kukabidhi  msaada wa kisima kwa zahanati hiyo.
 Malulu akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.
 Baadhi ya wakazi wa Tabata waliofika kwa kupata huduma za tiba katika Zahanati hiyo wakishiriki katika hafla hiyo.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dk Assenga Severine, akifungua pazia kuashiria kuzindua rasmi kisima katika Zahanati ya Tabata Nbc  Dar es Salaam.
 Ofisa Uhusiano kampuni hiyo,Dorris Malulu, akimkabidhi ufunguo wa kisima hicho Mwakilishi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Manispa ya Ilala, Dk. Assenga Severine,  kuashiria Uzinduzi wa Kisima ambacho kimejengwa kwa msaada wa TBL.
 Mkurugenzi Halmashauri ya Manispa ya Ilala, DK Assenga Severine na Ofisa Uhusiano kampuni ya Bia Tanzania Breweries (Tbl),Dorris Malulu wakionja maji ya kisima hicho baada ya Kuzindua kisima hicho.
 Mkurugenzi Halmashauri ya Manispa ya Ilala, Daktari Assenga Severine akimsaidia kumtwisha ndoo ya maji Ofisa Muuguzi wa zahanati yiho Flora Amos.
Ofisa Uhusiano kampuni ya Bia Tanzania Breweries (Tbl),Dorris Malulu, akimsaidia kumtwisha ndoo ya maji mmoja wa Wauguzi wa Zahanati hiyo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages