WANAMUZIKI na wadau wa muziki watakutana
Alhamisi hii saa 5 asubuhi kujadili namna ya kusaidia na kushiriki mazishi ya
mwimbaji Marehemu Amina Ngaluma (pichani, enzi za uhai wake).
Hilo litafanyika ndani ya ukumbi wa Vijana
Social Hall (jirani na Mango Garden), Kinondoni jijini Dar es ambapo
itaangaliwa namna nzuri ya kushirikiana na familia ya marehemu kuanzia hatua ya
kuupokea mwili hadi mazishi.
Mwili wa Amina Ngaluma aliyefariki nchini
Thailand Alhamisi iliyopita, utawasili jijini Dar es Salaam Ijumaa hii saa 3.30
usiku kwa ndege ya KLM. Mazishi
yatafanyika siku inayofuata (Jumamosi) mchana.
Mmoja wa waratibu wa kikao hicho cha Alhamisi
kinachoshirikisha pia Shirikisho la Muziki Tanzania, Mwinjuma Muumin, amesema
msiba huu umechukua muda mrefu, familia imeingia gharama kubwa katika kipindi
chote hiki na hivyo ni wakati muafaka sasa kwa wanamuziki na wadau wa
muziki kukutana na kuangalia namna ya
kuipunguzia mzigo familia ya marehemu.
Muumin amesema kuna mambo mengi ya msingi ya
kujadiliana katika kikao hicho na kwamba taarifa zote muhimu za mazishi ya
Amina Ngaluma zitatolewa hapo. Mwanamuziki Rashid Sumuni ambaye ni mume wa marehemu anatarajiwa kuhudhuria
kikako hicho.
Naye Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo
November amesema kikao hicho ni muhimu na kitafungua njia ya umoja na
mshikamano miongoni mwa wasanii hususan wanamuziki wa dansi
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269