Kikundi
cha mashabiki wa muziki nchini Iran walioiga wimbo maarufu wa
mwanamuziki maarufu wa Marekani Pharrell Williams, 'Happy' wamejipata
matatni baada ya kukamatwa na polisi.
Kanda
ya video waliyoirekodi wakiiga wimbo huo, inaonyesha vijana watatu na
wanawake kadhaa ambao hawakuwa wamejitanda mitandoa, wakicheza densi
kwenye barabara za nchi hiyo na kwenye paa za nyumba mjini Tehran.
Mkuu wa Polisi, Hossein Sajedinia, alisema kuwa kanda ya video inayoonyesha vijana hao wakicheza, imekiuka maadili ya jamii.
Kituo cha televisheni ya serikali kilionyesha vijana hao wakikiri makosa siku ya Jumanne.
Inaarifiwa
maelfu ya wananchi wa Iran wamekamatwa katika miaka 35 iliyopita
wakisherehekea na kujiburudisha kwa mambo ambayo serikali inaona kama ya
kukiuka maadili.
Hata
hivyo vijana hao wanaosema ni waigizaji wanadai kuwa walihadaiwa
kushiriki katika kanda hiyo na watu waliokuwa wanatafuta waigizaji
wakisema ulikuwa kama mtuhani kwao.
"waliniambia
kuwa wanatengeza filamu na kuwa walikuwa na kibali na ndio maana
nikakubali kushiriki,'' alisema mmoja wa vijana waliokamatwa.
Mtuhumiwa mwingine alisema walionasa kanda hiyo waliwaahidi kwamba hawataisambaza.
'Wamekiuka maadili'
Kulingana
na taarifa ambazo bado hazijathibitishwa, watu 13 walikamatwa kuhusiana
na kanda hiyo, ingawa idadi kamili ya waliokamatwa haijatangazwa rasmi.
Pharrel
aliyeteuliwa kwa tuzo la Oscar kwa wimbo wake huo mwaka huu ambao
umekuwa maaruufu sana duniani, alielezea kukasirishwa na hatua ya vijana
hao kukamatwa.
"yani siamini kama watoto hawa walikamatwa kwa kujaribu kueneza furaha,'' alisema Pharrell katika ukurasa wake wa Facebook.
Chini ya sheria za kiisilamu, sharti mwanamke ajitande kutoka kichwani hadi katika viganja vya mguu.
Polisi
ambao jukumu lao ni kuhakikisha kuwa sheria ya mavazi inafuatwa,
hushika doria mara kwa mara katika barabara za mji mkuu Tehran.
Kanda
hiyo ya "Happy we are from Tehran" ilionekana kwenye mtandao wa Youtube
tarehe 19 Mei na kufikia sasa imetazamwa mara 40,000.
Baadhi wametuma ujumbe wa kukejeli serikali ya Iran wakisema kuwa Iran ni nchi ambako ni hatia kwa mtu kuwa na furaha.
Wimbo
halisi wa Pharrell 'Happy' umepelekea maelfu ya watu kote duniani kuiga
video ya wimbo huo na kutengeza video zao wenyewe. Kutoka Kenya,
Marekani , Uingereza yaani nchi nyingi duniani tu, watu wameiga video
hiyo kwa kutengeza yao wenyewe.CHANZO BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269