Pichani ni Bw.Joseph Magessa aliyetuhumiwa hivi karibuni na tukio la Nyoka aina ya Chatu.
SAKATA
la kukutwa na chatu eneo la sakina katika nyumba ya Joseph Magessa
limechukua sura mpya baada ya mhusika kuhojiwa na mtandao wa jamiiblog
huu kuhusiana na tukio hilo.
Aidha chatu huyo ambaye alikutwa nyumbani
kwa mmiliki huyo hivi karibuni imeelezwa tuhuma hizo sio za kweli bali
ni njama za kumuharibia tu na tukio hilo ni la kutengenezwa na watu kwa
lengo la kumchafulia jina lake.
Magessa
alisema kuwa ,ameshangazwa sana na tukio hilo kwani lilipotokea alikuwa
safarini yeye na mke wake , ndipo alipopigiwa simu kuhusiana na tukio
hilo na kuwataarifu huyo chatu auawe.
.
Pia, amedai kuwa hizo zinaweza kuwa njama za watu zilizolenga kumchafua na kwamba, suala hilo amemwachia Mungu kwani ndiye ajuaye ukweli.
Pia, amedai kuwa hizo zinaweza kuwa njama za watu zilizolenga kumchafua na kwamba, suala hilo amemwachia Mungu kwani ndiye ajuaye ukweli.
Aliongeza
kuwa, yeye hajawahi kuwa mshirikina wala mke wake bali wanachojua wao
ni kuwa wanamtumikia Mungu na yeye pekee ndiye ajuaye kila jambo na kuwa
mambo yote hayo yaliyotokea amemwachia Mungu ndiye atakayejibu.
Magessa alifafanua kuwa, ameshangazwa sana na taarifa
mbalimbali ambazo zimekuwa zikizushwa kwenye vyombo vya habari pamoja
na mitandao juu ya tukio hilo ila yeye amenyamaza kimya na amemwachia
Mungu kwani ndiye ajuaye kila kitu.
KUHUSU KUTENGWA KWAKE KANISANI .
Aidha
akizungumzia kuhusiana na swala la kutengwa kwake na Kanisa katoliki
alisema kuwa huo ni uongo na uzushi hakuna kitu kama hicho kwani
wanamwelewa vizuri sana tabia yake na kuwa hana tabia ya ushirikina.
‘Tena
waumini wa kanisa katoliki watakuja kufanya jumuiya nyumbani kwangu na
tayari kuna masalaba pale kama kweli ningekuwa nimefanya hivyo leo hii
wangefuata nini hapa kanisani’alisema Magessa.
Naye
mkewe Selina Magessa , akizungumza na jamiiblog kuhusiana na tukio hilo
alisema kuwa.tangu ameanza kuishi na mumewe miaka mingi hadi sasa hivi
,hajawahi kusikia wala kuona
vitendo vya ushirikina.
“Niko na mume wangu miaka mingi, sijawahi kusikia kuwa anafuga nyoka ndani wala sijafiwa na mtoto yeyote, wote watatu wapo ila nashangaa kusikia kauli kwamba mume wangu aliagiza nyoka asiuawe kwa kuwa ni mtoto wake ama mama yake mzazi,” alisema Selina.
Alisema kuwa , kwa sasa hivi ni muda wao kupumzika na kutafakari mambo yao sio wakati wa kuzungumzia swala hilo tena kwani wamechishwa na maneno kila mahali ili wanachofanya ni kumwachia mungu pekee ndiye ajuaye.
Hata
hivyo ,Magessa anapenda kuwaelezea watanzania kwamba huyo chatu sio wa
kweli ni wa kurushwa kwenye fensi yake ili amchafulie kwani
chatu wa ukweli asingeweza kuburuzwa hadi kanisani kwani kila mtu
anamwelewa mnyama huyo jinsi alivyo mkali ,kwa hiyo hizo ni njama tu za
kuharibiana kwenye maisha .
Hivyo alisema kuwa, kusisitiza kuwa anaombwa watanzania wamwelewe kwani chatu wa ukweli wanafahamika.
ATOA RAI KWA VYOMBO VYA HABARI.
Aidha
alivitaka vyombo hivyo kuelimisha jamii badala ya kupotosha ukweli wa
jambo kama ambavyo sakata hilo limezua sura tofauti kwa watanzania .
‘mnajua
nyie ndio vyombo tunavyovitegemea kwa jamii ,sasa mkiandika vitu
ambavyo hamna uhakika navyo mnategemea italeta picha gani kwa jamii ya
watanzania ‘alisema Magessa.(CHANZO Pamela Mollel jamiiblog)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269