Breaking News

Your Ad Spot

Jun 25, 2014

RAIS KIKWETE ATUA MALABO, EQUTORIAL GUINEA, KUHUDHURIA MKUTANO WA 23 WA UMOJA WA AFRIKA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mji mkuu wa Equatorial Guinea wa Malabo leo Juni 24, 2014 kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Africa –African Union (AU).

Akiwa Malabo, Mheshimiwa Rais Kikwete pia atakuwa Mwenyekiti wa kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa AU kitakachojadili mazingira. Rais Kikwete na ujumbe wake anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Equatorial Guinea Mhe Vicente Ehate Tomi alipowasili  katika katika uwanja wa ndege wa Malabo, Equatorial Guinea, leo Juni 24, 2014
PICHA NA IKULU
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Malabo, Equatorial Guinea, leo Juni 24, 2014

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages