Afisa
Habari wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA), Mhandisi Yesambi
Shiwa (Kulia) akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa TMAA kwa Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab
Mkwizu (Kushoto) wakati alipotembelea kwenye Banda la TMAA wakati wa
Maadhimisho ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini
Dar es Salaam.
Mashine
ya kisasa ya kupimia ubora wa sampuli za madini ikioneshwa kwenye Banda
la TMAA wakati wa Maadhimisho ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya
Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab
Mkwizu (Kushoto) akizungumza na watumishi wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini
(TMAA) alipowatembelea kwenye Banda lao. Wanaomsikiliza ni Afisa
Habari, Mhandisi Yesambi Shiwa (Kulia) na Afisa Utumishi, Bibi Fatma
Chondo (Katikati).
Makaa
ya mawe yakioneshwa kwenye Banda la TMAA wakati wa Maadhimisho ya
Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya sampuli za madini yapatikanayo nchini yakioneshwa kwenye Banda la
TMAA wakati wa Maadhimisho ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab
Mkwizu (Kushoto) akihimiza kufanya kazi kwa uzalendo kwa watumishi wa
Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) alipowatembelea kwenye Banda
lao. Picha zote na:Saidi Mkabakuli
Na Saidi Mkabakuli.
Serikali
imeupongeza Wakala wa ukaguzi wa madini nchini (TMAA) kwa kufanikiwa
kuokoa kiasi kikubwa cha madini yaliyokuwa yakitoroshwa kinyemela katika
viwanja vya ndege nchini hivyo kuokoa zaidi ya bilioni 15 zilizolipwa
kama mrahaba tangu ilipoanzisha ukaguzi maalum kwa wasafiri waendao nje
ya nchi.
Pongezi
hizo zimetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu alipokuwa akikagua utendaji kazi wa
Wakala katika maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Bw.
Mkwizu alisema kuwa kwa muda mrefu sasa wafanyabiashara wasio waaminifu
wamekuwa wakiitia hasara Serikali kwa kukwepa ulipaji wa kodi wa madini
yaendayo nje ya Tanzania kinyume na utaratibu uliowekwa.
“Hongereni
sana kwa kuweza kuokoa kiasi kikubwa cha madini yaliyokuwa
yakisafirishwa bila kufuata taratibu zetu za usafirishaji wa madini
yaendayo nje ya Tanzania,” alisema Bw. Mkwizu. Naibu Katibu Mkuu Mkwizu
aliwasihi viongozi na watumishi wa Wakala kuongeza uchapaji kazi na
uzalendo ili kuweza kukomesha kabisa tabia ya wafanyabiashara hao wasio
waaminifu.
Akikaribishwa
kwenye banda la Wakala kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na Afisa Habari
wa Wakala hiyo, Mhandisi Yisambi Shiwa, Bw. Mkwizu alijulishwa kuwa moja
kati ya mafanikio yaliyofikiwa na Wakala mara baada ya ukaguzi wa ziada
kwa wasafiri waendao nje ya Tanzania, ni pamoja na kubainika mamia ya
wafanyabiashara wa madini ambao wamekuwa wakitorosha kinyemela madini ya
thamani kubwa ya fedha bila kufuata taratibu.
“Katika
kuboresha utendaji kazi wa Wakala, tulitambulisha mpangokazi mpya wa
ukaguzi wa ziada katika viwanja vyetu vya ndege vikubwa vya Dar es
Salaam, Kilimanjaro na kile cha Mwanza lengo ni kubaini wafanyabiashara
wasio waaminifu na ndipo tulipobaini wizi huu,” alisema Mhandisi
Shiwa. Akizungumzia thamani ya madini hayo, Mhandisi Shiwa alisema kuwa
kufuatia ukaguzi huu, mpaka sasa Wakala imeweza kuokoa madini yenye
thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 15. “Ukaguzi huu
umesaidia kuokoa kiasi kikubwa cha madini yenye thamani ya shilingi
bilioni 15.3 hadi kufikia mwaka na hivyo kuiongezea serikali yetu mapato
ambayo yalikuwa yatoroshwe na wafanyabiashara hao wasio waaminifu,”
aliongeza.
Kwa
mujibu wa Mhandisi Shiwa, kiasi hiki cha fedha ni sehemu ya mrahaba wa
kisheria unaostahili kuchangiwa na wafanyabiashara hao kwa umiliki wao
wa madini hayo kabla ya kusafirisha nje ya nchi.
Mhandisi
Shiwa aliongeza kuwa katika kuendelea kudhibiti tabia hizi, Wakala kwa
kushirikiana na taasisi nyingine za serikali imekuwa ikishikilia na
kutaifisha madini yanayotiliwa shaka ama kumilikiwa isivyo halali
yanayopatikana katika viwanja hivyo.
Wakala
wa Ukaguzi wa Madini Tanzania ni Wakala wa Serikali ulioanzishwa tarehe
2 Novemba, 2009 chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura ya 245.
Tamko la Waziri la kuanzisha Wakala lilichapishwa kwenye Gazeti la
Serikali Namba 362 la tarehe 6 Novemba, 2009.
Lengo
la Wakala ni kuhakikisha kwamba, Serikali inapata mapato stahiki kutoka
kwenye shughuli za uzalishaji na biashara ya madini nchini kupitia
usimamizi na ukaguzi makini wa shughuli za uchimbaji, na kuhakikisha
kuwa shughuli hizo zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji
thabiti wa mazingira katika maeneo ya migodi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269