Breaking News

Your Ad Spot

Jul 25, 2014

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA YA UMAHIRI WA KUBAKA, KULAWITI NA KUTOBOA MACHO WATOTO SHINYANGA

Jacob Mayani  aliyehukumiwa kifungo cha maisha kwa kubaka, kulawiti na kutoboa macho watoto akipelekwa jela kutuimikia kifungo

NA MWANDISHI MAALUM, SINYANGA
Mtuhumiwa aliyekuwa akikabiliwa na kesi za ubakaji na kulawiti watoto katika Manispaa ya Shinyanga amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia katika kesi tatu tofauti zilizokuwa zinamkabili.

  Jacob Mayani au maarufu kwa jina la Boy mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa manspaa ya Shinyanga amehukumiwa vifungo vitatu vya maisha kwenye Mahakama ya  Hakimu mkazi Mfawidhi Shinyanga.

Jacob Mayani ambaye alifikishwa mahakamani kwa  kuhusika na  matukio tofauti ya ubakaji na kulawiti watoto chini ya miaka 10 sanjari na kuwatoboa macho amejikuta akiishia gerezani.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages