Mwanamke
raia wa Sudan aliyesamehewa adhabu ya kifo baada ya kubadili dini
amesafirishwa hadi nchini Italia baada ya kuwa kwenye ubalozi wa
Marekani mjini Khartoum kwa zaidi ya mwezi mmoja.Meriam Yahia Ibrahim
Ishag na familia yake waliondoka na ndege ya serikali ya Italia
wakiongozana na Waziri wa nchini Italia Lapo Pistelli Baba wa Meriam ni
muislamu na kwa Misingi ya sheria ya dini hiyo nchini Sudan Meriam pia
ni muislamu na hawezi kubadili dini.
Meriam
mwenyewe alilelewa na mama yake ambaye ni mkristo na kusema kuwa
hajawahi kuwa muislamu.Pistelli Naibu waziri wa mambo ya nje wa Italia,
aliweka picha yake na Meriam kwenye ukurasa wake wa facebook akisema
kuwa wanaelekea kutua mjini Roma.
Mume wa Meriam Daniel Wani, ni mkristo,ana asili ya Sudani kusini na ana uraia wa Marekani. Mtoto wa
Meriam, Maya alizaliwa gerezani mwezi May, muda mfupi baada ya
kuhukumiwa kunyongwa hatua iliyosababisha ghadhabu dunia nzima. Aliachwa huru mwezi Juni baada ya kuwepo kwa mashinikizo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269