Breaking News

Your Ad Spot

Jul 19, 2014

CHADEMA YAANZA KUFA KIGOMA, VIONGOZI WA MKOA WAHAMIA CHAMA CHA ZITTO KABWE

???????????????????????????????
Viongozi wa CHADEMA Mkoa wakitangaza kujiuzuru, Jumai 18, 2014, kutoka kushoto ni Msafi Wamarwa aliyekuwa Katibu wa chama Mkoa, Ramadhani Kasisiko aliye kuwa Mwenyekiti wa chama Mkoa na Malumba Simba liyekuwa Katibu wa BAWACHA
…………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu,Kigoma
Dalili za kifo cha chama cha  CHADEMA katika mkoa wa Kigoma, zimezidi kuwa kubwa kufuatia viongozi muhimu wa chama hicho ngazi ya mkoa huo, kutangaza  kujiuzulu rasmi nyadhifa zao na uanachama wa chama hicho, jana, Julai 18, 2014.

Viongozi hao waliotangaza kujiuzuru nafasi zao katika chama hicho mbele ya waandishi wa habari ni Jafari Ramadhani Kasisiko ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama Mkoa,Msafiri Hussen Wamarwa amabye alikuwa katibu wa chama Mkoa pamoja na Malunga Masoud Simba alikuwa Kaibu wa Baraza la wanawake BAWACHA.

Akitangaza uamuzi kwa niaba ya wenzake aliyekuwa Mwenyekii wa CHADEMA Jafari Kasisiko alisema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kuona CHADEMA kimepoteza sifa ya kuwa chama cha demokrasia na kuwa chama cha wababe.

”Sifa iliyokuwa inaufanya ubaki CHADEMA ni kwakuwa kilikuwa ni chama cha dempkrasia lakini hivi sasa kimeshapoteza hiyo sifa na kuwa chama cha kibabe na kinachokiunga misingi ya demokrasia hatuna sababu ya kuendelea kubaki katika chama hiki”alisema Kasisiko.

Kasisiko ambaye aliondoka chama cha CCM mwaka 1985 na kukaa nje ya siasa kwa muda kabla ya kujiunga na CHADEMA mwaka 1994.

”Kwa mfano wa demokrasia inayokiukwa CHADEMA kipindi kile aliyekuwa Naibu katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe Zitto alipotaka kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA alivuliwa wadhifa wake baada ya  kutangaza nia sasa pale Zitto kosa lake nini?alihoji lakini ukipitia Katiba ya CHADEMA hakuna sehemu inayokataza mwanachama kugombea nafasi ya uenyekiti”

”Kwahiyo katika CHADEMA sasa hivi nafasi ya uenyekiti ni kitu nyeti sana hastahili mwanachama yeyote kugombea”alisema Kasisiko.
 
Alisema kuwa pamoja na kuwa wamechukua muda mrefu kabla ya kuangaza uamuzi wao huo walikuwa na sababu za msingi zilikuwa zinawafanya wasiangaze haraka uamuzi huo,lakini tangu Zitto alivyovuliwa madaraka yake walikuwa hawana imani tena na chama kwasababu hawezi kuwa ndani ya chama ambacho ni mamlaka ya fulani.

Naye aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa chama hicho Msafiri Wamarwa alisema kuwa kwa ridhaa yake toka moyoni bila ya kushawishiwa na mtu ameamua kuondoka CHADEMA na kabla ya uamuzi huo alikaa chini na kutafakari sana na kuona njia sahihi ni kutoka CHADEMA kwakuwa chama hicho hakina faida kwa wananchi.
 
 Baada ya kujiuzulu uongozi na uanachama toka CHADEMA aliyekuwa Mwenyekii wa chama hicho Mkoa Ramadhani Kasisiko anajiunga na chama kipya cha cha siasa cha Allience  for Change  and Trasparency (ACT) ambacho kinaaminika kuasisiwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe, lakini wenzake wamesema bado wanatafuta chama makini cha kujiunga nacho.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages