Breaking News

Your Ad Spot

Jul 22, 2014

MAMA ADAIWA KUMUUA MWANAE WA MIEZI MIWILI KUTOKANA NA MZAZI MWENZIE KUTOTOA MATUNZO

Na Chibura Makorongo, Shinyanga
Mama mmoja mkazi wa Kijiji cha Nyasubi, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Rhoda Idetemya (18),  anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumnyonga mtoto wake mwenye umri wa miezi miwili kwa madai ya kukosa fedha za kumtunza mtoto huyo.

Imeelezwa kwamba baada ya kumnyonga mtoto huyo ambaye ametambuliwa kwa jina la Elizabeth Idetemya mama huyo alimtumbukiza kwenye kisima cha maji ya kunywa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea jana, Julai 21, mwaka huu, mida ya saa moja jioni

Kamanda Kamugisha alisema mwili wa mtoto huyo uligunduliwa na Ada Patrick (25) mkazi wa kijiji hicho cha Nyasubi wilayani humo wakati akichota maji kwenye kisima hicho cha maji ya kunywa na ndipo alipo uona mwili wa mtoto huyo ukielea.

Alisema baada mwanamke huyo Ada Patrick kuuona mwili huo alitoa taarifa polisi wilayani Kahama na polisi walipofika eneo la tukio waliukuta mwili wa mtoto huyo ukiwa ndani ya kisima cha maji na kuuopoa.
 Kamanda Alisema kutokana na mauaji hayo mama mzazi wa mtoto huyo Rhoda Idetemya (18) alikimbia ambapo Jeshi hilo lilifanya juhudi za kumsaka na kumkuta ndani ya gari la abiria liendalo wilayani Bukombe mkoani Geita akijaribu kuitoroka.
Kamugisha alitaja chanzo cha mauaji hayo kuwa ni mgogoro uliokuwepo baina ya mama huyo na mzazi mwenzake ambaye hakubainika jina lake kwa madai kuwa baada ya kuzaliwa mtoto huyo hawala yake (BWANA YAKE) alikuwa hatoI pesa ya matumizi hali iliyompelekea kushindwa kumhudumia mtoto huyo na kuchukua uamuzi kwa kumua.
Kwa taarifa zaidi ya jeshi la polisi mkoani Shinyanga lilimhoji mwanamke huyo ambapo amedaiwa kukiri kufanya mauaji hayo kutokana na kukosa pesa ya kumhudumia mtoto wake huku jeshi hilo likimshikilia mwanamke huyo kwa tuhuma za maji hayo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages