Breaking News

Your Ad Spot

Jul 10, 2014

MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI KWA TIKETI YA FRELIMO ATETA NA KATIBU MKUU WA CCM, ABDULRAHMAN KINANA, DAR


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasili na mgeni wake, Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama Cha Ukombozi cha FRELIMO, Filipe Nyusi, kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam, ambako walifanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa. Katika ziara yake ya siku tatu, pamoja na mambo mengine Nyusi atasaka kura kwa Wananchi wa Msumbiji waishio Tanzania
 Kinana akimtambulisha kwa Nyusi, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Waziri wa Katiba na Sheria,  Dk. Asha-Rose Migiro, kabla ya kuanza mazungumzo yao kwenye hoteli ya Golden Tulip Dar es Salaam, leo, Julai 10, 2014.
 Nyusi akieleza kwa waandishi wa habari lengo la ziara yake hapa nchini, ambapo alieleza mikakati ya chama chake cha FRELIMO kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu ambao kampeni zake zinaendelea. pamoja naye ni Kinana na Dk. Asha-Rose Migiro.
 Kinana akiwa katika mazungumzo na mgeni wake, Filipe Nyusi (kulia)
Ujumbe wa mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya FRELIMO ukiendelea na mazungumzo hayo leo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages